Main Title

source : ABNA
Jumatano

8 Januari 2020

04:08:38
1000363

Ainul Asad, ngome kuu na kubwa kuliko zote zenye kumilikiwa na Marekani katika ardhi ya Iraq.

Shirika la habari AhlulBayt (as): Ainul Asad, ngome kuu na kubwa kuliko zote zenye kumilikiwa na Marekani katika ardhi ya Iraq.

Ngome hii imekuwa ikitumika kama uwanja wa ndege mkuu kwa majeshi ya Marekani nchini humo, na hata mwa wa jana Rais Donald Trump katika sherehe za kuwapongeza Wanajeshi wake alifikia katika ngome hii.

Uwanja pekee kwa ajili ya kutua ndege una urefu wa mita zipatazo 4000, huku eneo lote likiwa ni mita 188 kutokea usawa wa bahari.

Jeshi la Sepah lakiri kushambulia:

Katika taarifa kutoka ndani ya Majeshi ya Sepah nchini Iran, inaelezwa kwamba Jeshi hilo limekiri na kukubali kuhusika na shambulio la alfajiri ya leo, huku wakitanabahisha kuendelea na visasi endapo tu Marekani itachukua hatua yeyote.

“...Tunatoa tahadhari kwa nchi zote ambazo zitatoa maeneo yake kuipatia nchi ya Kigaidi ya Marekani kwamba hatutaacha kuzifanya ndio lengo la makombora yetu...” Ilisema taarifa kutoka Jeshi la Sepah.

mwisho/290