Main Title

source : ABNA
Jumatano

8 Januari 2020

06:11:01
1000448

“hatupo katika kutafuta vita, kilichofanyika ni kisheria kabisa” – Zarif

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw Javad Zaref, ametanabahisha kwamba nci yake haipo katika harakati za kutafuta vita, na kilichotokea alfajiri ya leo ni kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Mataifa chini ya kipengele cha 51.

Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as):

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw Javad Zaref, ametanabahisha kwamba nci yake haipo katika harakati za kutafuta vita, na kilichotokea alfajiri ya leo ni kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Mataifa chini ya kipengele cha 51.

“Iran imechukua hatua munasibu katika hili, ni kwa mujibu wa kifungu cha 51 katika vipengele vya Umoja wa Mataifa. Na kambi ambayo imekuwa ikihusika na kushambulia raia wetu ndiyo ambayo tumeilenga..” aliandika Zaref katika ukurasa wake wa Twitter.

Kama ambavyo katika maelezo yake Zaref ametilia mkazo swala la kutokuwa na nia ya kupigana, lakini haina maana kwamba watakaa kimya dhidi ya mashambulizi ya adui.

“.....Hatutafuti vita, ila katika kukabiliana na kila aina ya shambulizi ni lazima tujilinde...” alitilia mkazo Zaref.

Hayo yamekuja baada ya Majeshi ya Iran kushambulia kambi za Marekai nchini Iraq alfajiri ya leo, ambapo mpaka sasa zaidi ya Wanajeshi 200 wa Marekani wamekuwa wahanga wa mashambulio hayo.