Main Title

source : ParsToday
Jumatano

8 Januari 2020

08:13:05
1000509

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inachukua hatua kwa ajili ya kudhamini usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi na Oman pia inashirikiana na Tehran katika uwanja huo.

(ABNA24.com) Yusuf bin Alawi ametoa mkono wa taazia kwa serikali na wananchi wa Iran kufuatia kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na kueleza kuwa Kamanda Soleimani alihudumu pakubwa na kufa kwake shahidi kumekuwa na taathira kwa wote.

Bin Alawi ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran 2020. Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman ameeleza kufurahishwa na kushiriki nchi yake katika Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran na kueleza kuwa: Viongozi wa Marekani wanataka kupunguzwa hali ya mivutano katika mazungumzo ambayo wamekuwa wakifanya siku zote na Oman.  

Jukwaa la Mazungumzo ya Tehran 2020 limeanza leo katika Kituo cha Utafiti wa Kisiasa na Kimataifa cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, rais wa zamani wa Afghanistan na wageni kutoka Russia, Iraq, China, Umoja wa Ulaya, Pakistan, India, Qatar, Kuwait na Yemen.  

Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria leo wakati wa kuanza jukwaa hilo la mazungumzo kuhusu jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Kamanda Qassem Soleimani na kusisitiza kuwa taathira za mauaji hayo ya kigaidi ya kiongozi wa ngazi ya juu wa kijeshi wa Iran zitaikumba Marekani hivi karibu au kwa kuchelewa kuanzia Mashariki hadi Magharibi.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ambaye alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi na wenzake wanane Ijumaa alfajiri iliyopita katika shambulio la anga la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq.

..........
340