Main Title

source : ParsToday
Jumatano

8 Januari 2020

08:13:08
1000510

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa mwisho wa kuwepo kwa ushari Marekani katika eneo la Asia Magharibi umeanza na kueleza kuwa, taathira za kuuliwa kigaidi kiongozi wa kijeshi wa ngazi ya juu wa Iran zitaidhuru Marekani kwa kuchelewa au hivi karibuni kuanzia Mashariki hadi Magharibi.

(ABNA24.com) Akizungumza Jumanne katika Jukwaa la Mazungumzo ya Kieneo hapa Tehran (Tehran Dialogue Forum), Muhammad Javad  Zarif ameashiria jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kueleza kuwa, Marekani kwa mara nyingine tena imewathibitishia watu wote kwamba haiheshimu kanuni na sheria zozote za kimataifa.

Zarif ameongeza kuwa kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani si tu ni shambulio dhidi ya mamlaka ya kitaifa ya Iraq na ni mauaji ya kinyama dhidi ya kamanda mkuu wa Iran bali ni kitendo cha kushambulia mhimili wa kudhamini usalama katika eneo la Asia Magharibi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Rais asiye na adabu na fidhuli wa Marekani na Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni asiye na adabu kabisa mara hii wamecheza kamari kubwa kwa kumuua kigaidi Kamanda Soleimani. Amesisitiza kuwa Marekani itapokea jibu lake kwa wakati na sehemu munasibu ili kwa uchache ihisi maumivu.

Zarif ameyataja maoni potofu yaliyoathiri mlingano wa kieneo kuwa moja ya matatizo makuu katika kanda hii ya magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa mifumo ya kifikra na kinadharia ambayo imetwishwa kwa eneo la Asia Magharibi na kuenezwa na baadhi ya watu na nchi katika ama kwa kujua au kutojua, ni kuwa silaha za Marekani na vita ndivyo vinavyoweza kuimarisha amani. 

.........
340