Main Title

source : ParsToday
Jumatano

8 Januari 2020

08:13:11
1000511

Kuakisiwa pakubwa shughuli ya kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani

Mahudhurio ya jana ya mamilioni ya wananchi wa mji mkuu wa Iran, Tehran katika shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani pamoja na mashahidi wengine wa muqawama yameakisiwa pakubwa na vyombo vya habari katika eneo la Asia Magharibi na nje ya eneo hili.

(ABNA24.com) Jana Jumatatu wakazi wa Tehran walitengeneza hamasa kubwa kutokana kwa kujitokeza kwa mamilioni na kuonyesha ni kwa kiasi gani wanawathamini mashujaa wa kitaifa. Hamasa hiyo kubwa imeakisiwa pakubwa na vyombo vya habari katika maeneo mbalimbali ya dunia vikiwemo vya Asia Magharibi ambavyo vimetumia ibara mbalimbali kuakisi tukio hilo la aina yake kama "Mawimbi Makubwa ya Wananchi", "Bahari ya Waombolezaji" na "Safu ya Kilomita Kadhaa ya Wairani". Kiujumla tunaweza kugawanya tathmini na uchambuzi wa tukio hilo katika makundi kadhaa.

Kundi Kwanza, limeyataja marasimu ya jana ya kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani na mashahidi wengine kuwa ni "tukio la kihistoria" na ni kwa sababu hiyo ndio maana limewashangaza na kuwaacha vinywa wazi. Mtandao wa Habari wa Times of Israel umeandika: Shughuli hiyo ya maombolezo na usindikizaji ni kubwa zaidi baada ya ile ya kuusindikiza mwili wa Imamu Khomeini.

Kundi la Pili limesema kuwa, mahudhurio hayo makubwa yamedhihirisha umoja uliopo miongoni mwa wananchi. Mwandishi wa habari wa al-Monitor ameandika kuhusiana na suala hilo kwamba: Mimi sijawahi kushuhudia kitu kama hiki nchini Iran. Hata katika mikusanyiko na shughuli za kidini watu hawakusanyiki namna hii kama walivyojitokeza katika shughuli ya kumsindikiza na kumuaga Qassim Soleimani.

Kundi la Tatu limesisitiza kwamba, Luteni Jenerali Qassim Soleimani alikuwa mtu wa watu na alikuwa akipendwa mno. Mahudhurio hayo ya ya mamilioni watu siyo tu kwamba, yanaonyesha huba ya wananchi na hali yao ya kuthamini mchango wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani, bali yametoa pigo kwa vita vya kisaikolojia vya hivi karibuni vya vyombo vya habari vya kimataifa vilivyolenga kuharibu haiba ya kamanda huyu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).

..........
340