Main Title

source : ParsToday
Jumatano

8 Januari 2020

08:29:49
1000517

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa, majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatatoa jibu kali zaidi na kwa nguvu zote dhidi ya hatua yoyote ghalati na ovu ya Marekani.

(ABNA24.com) Meja Jenerali Muhammad Baqeri amesema hayo leo Jumatano ambapo ameashiria kuhusu operesheni ya ulipizaji kisasi iliyofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) dhidi ya Marekani na kusisitiza kuwa, "Mashambulizi hayo ya makombora ya balestiki ya Iran dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Iraq ni sehemu ndogo sana ya uwezo mkubwa wa kijeshi wa taifa hili."

Amebainisha kuwa, wakati umefika kwa maafisa wa Marekani kufahamu na kutambua uwezo mkubwa wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu, na wachukue hatua sahihi ya kuondoa vikosi vya jeshi lao la kigaidi katika eneo.

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran ameeleza bayana kuwa, Jamhuri ya Kiislamu katu haigopi vita ikilizimika kuingia vitani kwa ajili ya kuwadhaminia usalama raia na kulinda mamlaka yake ya kujitawala, ingawa kiuhalisia haipendi vita.

Ameongeza kuwa, vikosi vyote vya Iran viko tayari kutoa majibu makali kwa uchokozi na uadui wowote itakaofanyiwa na utawala wenye kupenda shari wa Marekani na waitifaki wake.

Alfajiri ya leo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limevurumisha makumi ya makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi nchini Iraq, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.

..........
340