Main Title

source : ParsToday
Jumatano

8 Januari 2020

08:33:00
1000519

Marekani imekataa kumpa viza ya usafiri Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unaotazamiwa kufanyika Januari 9 mjini New York.

(ABNA24.com) Vyombo vya habari vya Marekani vimethibitisha habari hiyo ya utawala wa Washington kumnyima kibali hicho muhimu cha kusafiri mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran kwenda kushiriki mkutano wa Baraza la Usalama la UN.

Hatua hiyo ya Washington inakiuka 'Makubaliano ya Makao Mkuu ya 1947' ambayo yanaishurutisha Marekani kuwaruhusu nchini humo wanadiplomasia wa kigeni wanaokwenda kushiriki mikutano ya Umoja wa Mataifa.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema uhai wa Marekani unaelekea kufikia tamati na mchakato huo umeanzia hapa katika eneo hili la Asia Magharibi.

Dakta Zarif amesema hayo leo Jumanne katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Duru ya 23 ya Mazungumzo ya Tehran na kufafanua kuwa, "Kufikia tamati uwepo wa Marekani kumeanzia hapa eneo la Asia Magharibi, baada ya watawala wa Washington kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani."

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza bayana kuwa, Marekani kupitia mahesabu yake mabaya na maamuzi hasi ya kistratajia dhidi ya Iran na Asia Magharibi, imeiweka dunia katika hali ya ukosefu wa usalama.

Dakta Java Zarif ameongeza kuwa, "Akthari ya marais wa Marekani akiwemo Trump, kwa kutanguliza maslahi ya kisiasa ya ndani ya nchi, wamekuwa wakiwasha moto wa migogoro, uharibifu na umwagaji damu katika eneo na kote duniani."

..........
340