Main Title

source : ABNA
Jumatano

8 Januari 2020

17:18:25
1000671

Rais wa Marekani Donald Trump amehutubia muda mfupi uliopita na kudai kwamba mashambulizi ya makombora ya Iran hayakuwa na hasara yeyote kwa taifa lake.

shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa Marekani Donald Trump amehutubia muda mfupi uliopita na kudai kwamba mashambulizi ya makombora ya Iran hayakuwa na hasara yeyote kwa taifa lake.

Katika hotuba yake hiyo ambayo imekuja baada ya kuahidi kutoa kauli kunako mashambulizi ya alfajiri ya kuamkia leo (Jumatano), amesema kuwaambia Wamarekani kwamba wawe na amani kwani hakuna hata Mwanajeshi mmoja ambaye amepatwa na madhara ya shambulio hilo.

“...Kwa kutumia mfumo wetu wa kisasa ambao umetoa majibu mazuri, tumeweza kuwaokoa Wanajeshi wetu kwa wakati...” alisema Trump.

Siku chache zilizopita Trump alitishia kulipua maeneo 52 ya Iran ikiwemo maeneo ya kitamaduni, jambo ambalo katika mazunumzo yake ya leo amelitengua.

“...Katika kumalizia maongezi yangu napenda kuwaambia Wairan na viongozi wao kwamba sisi tunapenda muwe na mustakbali mzuri, na tunapenda kushirikiana na nchi zote ambazo zinapenda suluhu na makubaliano....” aliongezea Trump.

Wakati huohuo taarifa kutoka ndani ya Iran zinasema kwamba baada ya muda mfupi wataweza kuja na orodha kamili ya hasara na matokeo ya vifo vilivyotokana na mashambulizi hayo.