Main Title

source : ABNA
Jumatano

8 Januari 2020

17:36:05
1000678

Huku ulimwengu mzima ukiwa unasubiria na kufuatilia kwa umakini kabisa majibu ya Rais wa Marekani Bw Donald Trump baada ya kambi ya Jeshi la Marekani nchini Iraq kushambuliwa alfajiri ya leo na makombora ya Iran, hatimaye Trump amezungumza mbele ya waandishi wa habari na kuashiria baadhi ya mambo, huku akisema kuwa mashambulizi hayo hayajaacha athari yeyote kwa Wanajeshi wake.

shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: katika hali ambayo ulimwengu mzima ukiwa unasubiria na kufuatilia kwa umakini kabisa majibu ya Rais wa Marekani Bw Donald Trump baada ya kambi ya Jeshi la Marekani nchini Iraq kushambuliwa alfajiri ya leo na makombora ya Iran, hatimaye Trump amezungumza mbele ya waandishi wa habari na kuashiria baadhi ya mambo, huku akisema kuwa mashambulizi hayo hayajaacha athari yeyote kwa Wanajeshi wake.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo huenda yakawa ndio majibu yake kufuatia mashambulizi hayo, na ndio mambo ambayo ulikuwa ni msingi wa mazungumzo yake siku ya leo.

  1. Atahakikisha kwamba Iran inakumbana na vikwazo vikali zaidi
  2. Wito wake kwa Majeshi ya NATO kuwepo na kuhudhuria katika mizozo ifuatayo katika Mashariki ya Kati.
  3. Wito wake kunako kushirikiana na wengine mpaka wahakikishe kwamba wanamvuta Iran katika makubaliano mapya.

Trump hakutaka kabisa kuzungumzia swala la kushambulia Iran wala kambi zake kwa kudai kwamba anaitakia mema sana nchi hiyo.