Main Title

source : ABNA
Alhamisi

9 Januari 2020

06:57:31
1000801

Taarifa kutoka ndani ya Marekani zinasema kwamba kikundi cha wataalamu wa maswala ya saikolojia “World Mental Health Coalition” kimetoa tahadhari kufuatia hali ya Donald Trump kutokua nzuri kisaikolojia.

Video:

Taarifa kutoka ndani ya Marekani zinasema kwamba kikundi cha wataalamu wa maswala ya saikolojia “World Mental Health Coalition” kimetoa tahadhari kufuatia hali ya Donald Trump kutokua nzuri kisaikolojia.

Tahadhari hiyo imekuja baada ya wataalamu hao kumsoma na kulinganisha matukio ambayo yanaendelea katika masiku haya.

Tukio la Wabunge kutaka kumuwajibisha, shambulio la makombora ya Iran kushambulia kambi zake za Jeshi nchini Iraq, ni baadhi ya matukio yenye kuaminisha wataalamu hao tatizo la Kisaikolojia alio nalo kiongozi huyo.

Aidha katika taarifa yao wataalamu hao pia wamekitaka chama cha Rais huyo kuchukua hatua za haraka juu yake, kuchunguza afya yake, na hatimaye kuchukua maamuzi juu ya uwepo wake katika Ikulu ya Marekani kwa mazingira kama haya.

“Tumekuwa tukiashiria hili kwa muda sasa, hatua lazima zichukuliwe bila kuchelewa..” ilisema sehemu ya taarifa hiyo huku akiashiria kiande cha video ambacho Trump alikuwa akipata tabu ya kutamka maneno na kuhema kila wakati alipokuwa akizungumzia tukio la Iran kushambulia kambi za Marekani nchini Iraq.