Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

9 Januari 2020

07:34:35
1000842

Jibu kali la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa jinai na ugaidi wa vikosi vamizi vya Marekani

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, IRGC, mapema leo Jumatano alfajiri, katika kujibu jinai na ugaidi wa wanajeshi vamizi wa Marekani ambao walimuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, limevurumisha makombora ambayo yamelenga kituo cha anga cha jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani cha Ain al-Assad nchini Iraq.

(ABNA24.com) Kituo cha Ain al Assad ni kituo cha pili cha anga kwa ukubwa nchini Iraq baada ya kile cha Balad. Siku chache zilizopita, rais wa Marekani alizungumza kuhusu kituo hicho na kusema: "Marekani ina kituo cha kipekee na chenye zana  ghali na za kisasa za kivita nchini Iraq ambacho ujenzi wake umegharimu mamilioni ya dola. Kutokana na tulivyogharamika katika ujenzi wa kituo hicho hatuwezi kuondoka hadi pale Wairaqi watakapolipa gharama za ujenzi wake."

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC limetoa taarifa na kuionya Marekani isithubutu kuibua chokochoko zaidi la sivyo itakumbwa na jibu kali na la kuogofya la Iran.

Taarifa hiyo ambayo imetolewa mapema leo asubuhi pia imetoa onyo kali kwa nchi zozote ambazo zimetoa idhini kwa jeshi la kigaidi la Marekani kujenga vituo katika ardhi ya nchi hizo kuwa, shambulizi lololote la Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambalo litatekelezwa kutokea katika vituo hivyo litapelekea vituo hivyo kulengwa.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha katika taarifa hiyo limesema linauhesabu utawala wa Kizayuni wa Israel kama mhusika wa jinai za utawala unaotenda jinai wa Marekani. Aidha taarifa hiyo imetoa nasaha kwa watu wa Marekani, wachukue hatua za kuzuia hasara zaidi kwa kutaka wanajeshi wa Marekani walio katika eneo warejee nyumbani na kwa kuzingatia chuki inayoongozeka dhidi ya utawala wa Trump ulio dhidi ya wananchi, wasiruhusu maisha ya wanajeshi wao yanedelee kuwa hatarini.

Sisistizo la Iran kuhusu jibu kali kufuatia ugaidi wa Marekani ni haki ya kisheria na ni dharura katika kudhamini usalama wa eneo.

Brigedia Jenerali Ismail Kowsari, Naibu Kamanda wa Kituo cha Tharallah cha IRGC katika mahojiano na Shirika la Habari la Mehr ameashiria shambulizi la makombora la IRGC katika kituo cha anga cha wanajeshi wa kigaidi wa Marekani huko Ainul Assad katika mkoa wa Al Anbar magharibi mwa Iraq na kusema: "Kama ilivyosemwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kutoa kauli ambayo haikuitekeleza."

Naye Meja Jenerali Hussein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, siku ya Jumanne katika maziko ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani ameashiria takwa la taifa la Iran kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilipize kisasi na itoe jibu kali ambalo litapelekea waliomuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC wajute.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine wanane, walishambuliwa tokea angani na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote wakafa shahidi katika tukio hilo.

Usalama ni takwa la pamoja la nchi zote za eneo; lakini kile ambacho tumekishuhudia katika miongo ya hivi karibuni katika eneo ni ukosefu wa usalama ambao chimbuko lake ni Marekani na tawala fisadi na za shari katika eneo.

Kuna ushahidi wa wazi kuwa,  uwepo wa Marekani ni chanzo cha ukosefu wa usalama na utulivu katika eneo.

Iwapo jinai ya Donald Trump haitajibiwa vikali, ataendelea kutoa vitisho kwa wote katika maeneo yote ya dunia. Kwa miaka mingi sasa, uwepo wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq haujawa na matokeo yoyote ghairi ya chuki na kuongezeka mifarakano na misuguano baina ya mataifa ya eneo. Kwa msingi huo lazima Trump abebeshwe dhima ya ugaidi wake.

Usalama wa eneo ni hitajio la pamoja na haiwezekani nchi moja ikawa na usalama na wengine wakose usalama. Iran haiwezi kunyamazia kimya jinai za kigaidi, vitisho na uvurugaji unaotekelezwa na Marekani. Ni kwa msingi huo ndio Iran ikatuma barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa, Iran haitaki vita na inatahadharisha kuhusu uchokozi na chokochoko zozote za kijeshi dhidi yake.

...........
340