Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

9 Januari 2020

07:34:36
1000843

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema taifa la Iran limejiandaa na kujizatiti barabara mkabala wa madola ya kibeberu duniani.

(ABNA24.com) Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameashiria kuhusu hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kuvurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH ambapo amesisitiza kuwa: Jibu hilo la Iran ni sawa na kuizaba tu kibao Marekani.

Amesema, "Kibao kilizabwa usiku wa kuamkia leo, lakini cha muhimu zaidi ni kuwa, uwepo wa Marekani katika eneo unaelekea kufikia tamati."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo alipokutana na wakaazi wa mji mtakatifu wa Qum, kusini wa mji mkuu Tehran ambapo ameeleza bayana kuwa, jibu la leo asubuhi la Iran la kulipiza kisiasa mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni sehemu ndogo sana ya uwezo mkubwa Iran.

Kadhalika Ayatullah Ali Khamenei amemtaja shahidi Qassem Soleimani kama shakhsia shujaa katika medani za vita na mtu aliyekuwa na busara na hekima katika uga wa siasa.

Wakati huohuo, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wakati umefika wa kuikata miguu Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Duru za habari zimeliambia shirika la habari la Tasnim la Iran kuwa, kwa akali wanajeshi magaidi 80 wa Marekani wameuawa kufuatia kuvurumishwa makombora hayo ya Iran katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ain al-Assad katika mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa Iraq.

Habari zaidi zinasema kuwa, makombora yote yaliyovurumushwa na SEPAH yalipiga shabaha na wala hakuna hata kombora moja lililotunguliwa.

...........
340