Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

9 Januari 2020

07:34:36
1000844

Zarif: Iran imeshambulia kambi za Marekani nchini Iraq kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha UN cha haki ya kujilinda

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia hatua iliyochukuliwa leo na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ya kuwashambulia magaidi wa Kimarekani katika kambi ya kijeshi ya Ain al Asad nchini Iraq na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa jibu hilo kali kwa kutegemea kifungu nambari 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa cha haki ya kujilinda.

(ABNA24.com) Dk Mohammad Javad Zarif ameandika hayo leo Jumatano katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechukua hatua sahihi kabisa ya haki ya kujilinda na imeshambulia kambi ambayo imetumika kuwashambulia kiwoga wananchi na viongozi wa ngazi za juu wa Iran.

Amebainisha kuwa, Iran haina nia ya kushadidisha vita lakini iko imara kujilinda na kujihami mbele ya shambulio lolote lile la adui.

Usiku wa kuamkia leo Jumatano, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limezipiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za Marekani nchini Iraq ikiwa ni kujibu jinai ya kigaidi iliyiofanywa na askari vamizi wa Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

Mapema jana Jumanne, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema, ulipizaji kisasi wa taifa la Iran kwa damu ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha SEPAH utakuwa mkali, madhubuti, wa kutisha na wa kumfanya adui ajute.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, hicho ni kibao cha uso tu walichopigwa Wamarekani na kwamba ulipizaji hasa wa kisasi hicho, ni kutoka wanajeshi wote wa Marekani katika eneo hili.

............
340