Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

9 Januari 2020

07:42:43
1000846

Sisitizo la Kiongozi Muadhamu la udharura wa kuhitimishwa uwepo haribifu wa Marekani Asia Magharibi

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asubuhi ya leo amekutana hapa mjini Tehran na maelfu ya wananchi kutoka mji wa Qum kwa mnasaba wa kukaribia kumbukumbu ya Harakati ya Kihistoria ya Dei 19 iliyosadifiana na Januari 1978 ambapo sanjari na kubainisha kubainisha sifa maalumu za kishakhsia za Luteni Jenerali Qassim Soleimani ametoa tathmini jumla kuhusiana na matukio ya eneo na ustawi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

(ABNA24.com) Akiendelea na hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mashambulio ya makombora dhidi ya kambi mbili za kijeshi za Marekani huko nchini Iraq na kusema kuwa kibao kilizabwa usiku wa kuamkia leo, lakini makabiliano makuu na muhimu zaidi yanapaswa kuwa ni dhidi ya uwepo wa kifisadi na haribifu wa Marekani katika eneo. Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) usiku wa kuamkia leo lilivurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH. Afisa mmoja katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ametangaza kuwa, kwa akali wanajeshi magaidi 80 wa Marekani wameuawa na wengine takribani 200 kujeruhiwa katika mashambulio hayo.

Tajiriba imeonyesha kuwa, uwepo wa kijeshi wa Marekani na kutuma nchi hiyo vikosi vyake vya kijeshi katika nchi kama Iraq na Afghanistan ni chanzo cha matatizo mengi ya eneo, na Washington ingali imeng'ang'ania kuendelea na mwenendo huu sambamba na uingiliaji wake wa masuala ya ndani ya nchi za eneo hili. Hata hivyo hii leo mazingira ya eneo na mahesabu ya kisiasa na kijeshi yamebadilika, kwani wananchi na serikali zilizoingia madarakani kwa ridhaa ya wananchi katu hazikubaliani na mwenendo huu. Hii maana yake ni kuibuka mageuzi muhimu na ya kimkakati katika eneo na hata katika uga wa kimataifa.

Kuhusiana na hilo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kusambaratishwa mipango haramu ya Marekani katika Asia Magharibi ni mfano wa wazi wa tadibiri na ushujaa wa shahidi Qassim Soleimani. Akibainisha nafasi athirifu na isiyo na mithili ya Luteni Jenerali Qassim Soleimani kuhusiana na kadhia ya Palestina, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kuwa: Wamarekani walikuwa wakifanya njama ili kadhia ya Palestina isahauliwe na kuhakikisha Wapalestina wanakuwa katika mazingiira ya udhaifu ili wasiwe na uthubutu wa mapambano, lakini shakhsia mkubwa (Qassim Soleimani) aliwashika mkono Wapalestina na akawapa ujasiri na uwezo wa kupambana.

Kushindwa operesheni kubwa na hujuma za Wazayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza katika miaka ya hivi karibuni, ni ukweli ambao umegeuka na kuwa jinamizi kwa Marekani na viongozi wa Wazayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Hii kwamba, katika hujuma na mashambulio ya hivi karibuni ya Wazayuni dhidi ya Gaza, wavamizi makatili walikuwa wakibembeleza usitishaji vita ufanyike leo leo na hata sio kesho, ni ishara ya wazi ya kubadilika mahesabu ya nguvu; na haya mabadiliko yanaonyesha kwamba, zama za satwa ya Marekani, uvamizi na ukatili wa madola fisadi katika Asia Magharibi zinaelekea ukingoni.

Uamuzi wa hivi karibuni wa Bunge la Iraq wa kufukuzwa majeshi ya Marekani nchini Iraq ni hatua ambayo imechukuliwa katika fremu hii. Majimui ya matukio haya yanaonyesha kuwa, mazingira yanayotawala hivi sasa katika eneo yamebadilika haraka mno kuliko hata ilivyokuwa ikidhaniwa na Marekani na waitifaki wake.

Kama alivyobainisha Ayatullah Khamenei ni kuwa, uadui huu wa Marekani si wa kipindi na zama fulani tu, bali ni wa daima na milele, na ni kosa kubwa kudhani kwamba, kuna siku uadui wa Marekani dhidi ya Iran utafikia kikomo.

Hii leo maadui wa Mapinduzi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ni mjumuiko wa Marekani, Uzayuni, waporaji wa dunia na watumiaji mabavu ambapo uadui wao ni dhidi ya asili ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ambao umesimama kidete na imara kukabiliana na ubeberu.

Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akasisitiza kuwa, kuna haja ya kusimama kidete dhidi ya adui na njama zake zote katika nyanja zote iwe ni kijeshi, kiusalama au kiuchumi na kielimu. Njia ya kukabiliana na njama hizi ni kudumisha umoja wa kitaifa, tadibiri, ushujaa na kutoogopa hata kidogo vitisho vya adui.

...........
340