Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

9 Januari 2020

07:42:43
1000847

Iran: Tuliipa taarifa serikali ya Iraq kuhusu operesheni ya makombora dhidi ya kituo cha kijeshi cha Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu iliipa taarifa serikali ya Iraq kuhusu operesheni ya makombora iliyofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ainul-Assad na kusisitiza kuwa: Tehran inaheshimu na kuthamini mno kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Iraq.

(ABNA24.com) Mohammad Javad Zarif ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari katika ubalozi wa Iraq mjini Tehran, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo na kumbukumbu ya mashahidi wa shambulio la kigaidi la hivi karibuni lililofanywa na Marekani; na akabainisha kuwa: Operesheni ya shambulio la makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ililenga kituo ambacho Marekani ilikitumia kutekelezea jinai yake ya kuwaua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq la Al-Hashdu-Sha'abi pamoja na wanamuqawama wenzao.

Dakta Zarif ametoa mkono wa pole pia kwa wananchi wa Iraq na kueleza kwamba: Kuuawa shahidi Luteni Jenerali Soleimani na Abu Mahdi Al-Muhandis kumeupa hakikisho na dhamana ya milele udugu na mshikamano wa wananchi wa Iraq na Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iraq na Iran katika kusindikiza na kuaga miili ya mashahidi hao watukufu yamewaonyesha walimwengu kwa mara nyingine kwamba damu ya mashahidi hao ni baraka kwa mataifa ya eneo na hatari na nakama kwa wakoloni na mabeberu.

Aidha amesema, hatua hiyo ya kipumbavu ya mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani itapelekea kuhitimishwa uwepo wa nchi hiyo katika eneo la Asia Magharibi na akabainisha kuwa, kuwepo Marekani katika eneo hili hakujaleta kitu chochote kile zaidi ya hasara na uovu.

...........
340