Main Title

source : ABNA
Alhamisi

9 Januari 2020

15:56:24
1000950

Huku habari za kutodhurika mwanajeshi yeyote wa Marekani katika shambulio la makombora ya Iran, kiongozi wa Jeshi la anga wa Jeshi la Mapinduzi la Iran amesema kuwa shambulio ilikuwa ni lazima litokee na kwamba mwanzo wa harakati kubwa sana katika ukanda wa Mashariki ya kati.

Akielezea kwa undani kunako shambulizi hilo, Bw Haji Zadeh amesema kuwa halikuwa lengo lao kuuwa au kujeruhi mtu, japokuwa hilo limetokea bila shaka.

“....Kama ingekuwa tuna lengo la kuua watu basi tulikuwa na uwezo wa kupanga shambulio ambalo lingeangamiza watu 500, na kama wangejaribu kujibu kwa mara nyingine basi hata mazingira yetu pia yangebadilika....” alinukuliwa Haji Zadeh.

Aidha katika mkutano wake huo na waandishi wa habari, Haji Zadeh aliweka wazi picha zenye kuashiria maeneo ambayo makombora yao yaliweza kufika pamoja na baadhi ya hasara zilizopatikana, jambo ambalo Marekani mpaka sasa imeendelea kuficha.