Main Title

source : ABNA
Ijumaa

10 Januari 2020

18:28:08
1001135

Majeshi ya ulinzi na usalama ya Kuwait yajiweka tayari kimapambano baada ya kuonekana kutokuwa na hali nzuli ya usalama ya Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya uhakika vinasema kuwa majeshi ya ulinzi na usalama ya kuwait yajiweka tayari kimashambulizi katika sehemu mbalimbali za kijeshi nchini humo, kufuatia hali mbaya ya usalama nchini Iraq.

Vyanzo makini vya Kuwait vimetangza kuwa kufuatia amri iliotolewa na wizara ya mambo ya ndani nchini humo kwamba majeshi yanatakiwa kujiweka tayari kimapambano dhidi ya maadui.

Amri hiyo imetolewa kufuatia hali mbaya ya usalama iliopo nchini Iraq, hususan baada ya matukio yaliotokea hivi karibuni nchini humo, kwa upande mwengine vyombo vya usalama vya nchini humo vinafuatilia kwa undani zaidi mipaka yake ya nchi kavu baharini na anga kwa lengo la kuhakikisha maisha ya wananchi wake yanakuwa salama.

mwisho/290