Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

11 Januari 2020

08:17:52
1001289

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mahesabu ghalati na yenye madhara makubwa ya Marekani yanatokana na kushindwa nchi hiyo kuielewa vizuri Iran na eneo la Asia Magharibi. Amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa huru na usikubali kuburuzwa na Marekani na kuifanya Iran ikate tamaa kikamilifu na umoja huo.

(ABNA24.com) Rais Rouhani alisema hayo jana Alkhamisi katika mazungumzo ya simu na Charles Michel, Mkuu wa Baraza la Ulaya na kuongeza kuwa, iwapo Umoja wa Ulaya unataka kuwa na mchango mzuri katika juhudi za kudumisha amani kwenye eneo hili, basi Tehran iko tayari kikamilifu kushirikiana nao.

Amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya unapaswa kuonesha kivitendo kuwa hauko pamoja na Marekani katika vitendo vyake vya kigaidi na kusisitiza kuwa, Marekani inalifanyia taifa la Iran ugaidi mkubwa wa kiuchumi kwa kuliwekea vikwazo taifa hili hata vya madawa ya wanadamu na chakula. Baya zaidi ni kwamba Marekani imemuua kigaidi kamanda mkubwa wa kijeshi wa Iran na hivyo imekanyaga sheria na kanuni zote za kimataifa.

Amesema, maandamano makubwa ya wananchi kuanzia Kashmir hadi Iraq na Lebanon ya kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni uthibitisho wa jinsi shujaa huyo alivyokuwa anapendwa sana na jinsi alivyotoa mchango mkubwa wa kudumisha amani na utulivu katika eneo hili.

Kwa upande wake, Mkuu wa Baraza la Ulaya amesema katika mazungumzo hayo ya simu na Rais Hassan Rouhani kwamba anatoa mkono wa pole kwa Iran kutokana na matukio ya hivi karibuni na kusisitiza kuwa, mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni matunda ya mazungumzo ya miaka 10 ndio maana Umoja wa Ulaya unafanya juhudi zake zote kuyalinda mapatano hayo ya kimataifa.

.........
340