Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

11 Januari 2020

08:17:54
1001290

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na viongozi wa nchi kadhaa jirani, nchi za Ulaya na Afrika kwamba Iran inaunga mkono amani na usalama lakini haitakaa kimya mbele ya vitimbi vya Marekani.

(ABNA24.com) Alkhamisi ya jana Rais Rouhani alifanya mazungumzo ya simu na viongozi wa nchi za Qatar, Uingereza, Italia, Afrika Kusini na Mkuu wa Baraza la Ulaya na kubadilishana mawazo nao kuhusu mauaji ya kigaii yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani na matukio ya baada ya muaji hayo ya kigaidi.

Katika mazungumzo yake na Amir wa Qatar, Rais Rouhani ameyataja mauaji ya kigaidi ya Jenerali Qassem Soleimani kuwa ni jinai kubwa iliyofanywa na serikali ya Marekani na kutoa wito kwa nchi zote duniani hususan nchi jirani kulaani jinai hiyo. Vilevile katika mazungumzo yake na Rais Cyll Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Rouhani ameeleza matumaini kwamba: Wamarekani watakomesha vitendo vyao viovu na iwapo watakariri makosa yao na kuhujumu maslahi ya Iran, basi watakabiliwa na jibu kali zaidi.

Mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia ya Rais Hassan Rouhani na viongozi wa nchi mbalimbali duniani baada ya hatua ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani yanaonesha kuwa, Iran inataka amani na usalama katika kanda ya magharibi mwa Asia na ulimwenguni kwa ujumla lakini haitazembea katika kulinda maslahi yake.

Suala la kulaani ugaidi wa serikali wa Marekani ni jukumu la nchi zote duniani kwa sababu kunyamazia kimya ugaidi huo ni tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa. Kuuliwa kigaidi afisa wa ngazi za juu wa jeshi la Iran ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kwa msingi huo nchi zinazopenda amani na zenye siasa huru zinalazimika kuchukua msimamo imara na wa wazi dhidi ya ugaidi huo wa serikali ya Marekani na kuiwajibisha nchi hiyo kuhusiana na ukiukaji wake wa sheria za kimataifa.

Wakati huo huo hakuna shaka kwamba, walimwengu wanazitaka duru za kimataifa zifuatilie ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Marekani na waamini kwamba, kuzembea katika suala hilo kunaihamaisha Marekani kukariri uhalifu kama huo, jambo ambalo lina madhara kwa nchi zote za dunia. Ni kwa sababu hiyo ndipo katika katika mazungumzo yake na Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Rouhani akasisitiza kuwa, kuna umuhimu kwa nchi zote kuchukua msimamo imara kuhusiana na mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Luteni Jenerali Soleimani na kusema: Kuna ulazima wa kuieleza Marekani kwamba dunia haikubali kabisa sera zake za kutenda jinai.

Vitendo na jinai za Marekani zinakiuka hati ya Umoja wa Mataifa na iwapo hakutakuwepo msimamo imara wa kupinga jinai hizo yumkini suala hilo likazidisha ukosefu wa amani, uvamizi, ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala ya nchi mbalimbali, kupanuka zaidi ugaidi na kukaririwa ugaidi wa kiserikali wa Marekani.

Hii leo ulimwengu unahitajia zaidi amani kuliko wakati wowote mwingine  na hapana shaka kuwa, mienendo na sera za kujichukulia maamuizi ya upande mmoja za Marekani zinakiuka sheria za Umoja wa Mataifa.

Vilevile mienendo ya Rais Donald Trump wa Marekani inatishia usalama na amani ya kimataifa na ni kwa sababu hiyo ndiyo maana baada tu ya mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kwa amri ya Trump, Alkhamisi ya jana Baraza la Wawakilishi la Marekani (Kongresi) lilipitisha mpango wa kupunguza mamlaka ya rais wa nchi hiyo Donald Trump katika masuala ya vita.

Tajiriba ya kuwepo askari wa Marekani katika nchi za Iraq, Afghanistan na maeneo mengine ya dunia na vilevile kujiondoa nchi hiyo katika makubaliano na mikataba ya kimataiva inaonsha kuwa, iwapo nchi nyingine za dunia hazitachukua msimamo imara dhidi ya sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za serikali ya Washington basi zitalazimika kulipa ghara kubwa sana.  

.........
340