Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

11 Januari 2020

08:33:38
1001293

Scott Ritter, aliyewahi kuwa mkaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani amelegeza msimamo na kuachana na vitisho vyake alivyovitoa hapo kabla dhidi ya Iran kutokana na kuhofia jibu kali la Tehran.

(ABNA24.com) Afisa huyo afisa wa zamani wa Marekani na wa Umoja wa Mataifa amezungumzia mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq baada ya kuuawa Luteni Jenerali Qassim Soleimani na kusisitiza kwamba, mashambulio hayo yameonyesha ni kwa namna gani Iran imejiandaa kutoa jibu kwa harakati yoyote ya Washington dhidi yake.

Scott Ritter ameendelea kusema kuwa: Iran haikuwa na nia ya kuwauwa wanajeshi wa Marekani kwa mashambulio yake hayo, lakini ilitaka kumuonyesha Trump uwezo wake wa makombora na azma yake thabiti.

Mkaguzi huyo wa zamani wa silaha wa Umoja wa Mataifa amebainisha kuwa, nukta muhimu kabisa ya hatua ya Iran ni namna ilivyorusha makombora yake na hii inaonyesha kuwa, ni kwa miaka mingi taifa hili limepiga hatua katika uwanja huo.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH lilivurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, usiku wa kuamkia Jumatano iiliyopita kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.

Wakati Marekani ikidai kuwa, hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa au kuuawa katika shambulio hilo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu linasema kuwa, zaidi ya magaidi 80 wa jeshi la Marekani wameangamizwa mashambulio hayo ya makombora.

..........
340