Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

11 Januari 2020

09:20:25
1001300

Rais Rouhani: Kosa la kibinadamu kutokana na vitisho vya Marekani ndiyo sababu ya kuanguka ndege ya Ukraine

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kosa la kibinadamu lililotokana na vitisho vya Marekani vya kushambulia maeneo nyeti nchini Iran ndiyo sababu ya kuanguka ndege ya abiria ya Ukraine karibu na Tehran.

(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani amesema hayo katika taarifa yake ya leo Jumamosi na huku akigusia tamko lililotolewa na Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Iran kuhusu ajali hiyo, ameelezea kusikitishwa sana na ajali hiyo na kutoa mkono wa pole kwa mataifa, tawala na familia za wahanga wa ajali hiyo akisema: Baada ya utawala vamizi wa Marekani kuzusha hali ya vitisho dhidi ya taifa la Iran, majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliwekwa kwenye hali ya tahadhari kubwa ya kujilinda na shambulizi lolote la Marekani na kwa masikitiko ni kwamba katika hali hiyo ya wasiwasi mkubwa, kulitokea kosa la kiibinadamu na kusababisha maafa makubwa ya kupoteza maisha makumi ya watu wasio na hatia.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, uchunguzi unaendelea kuhusu sababu zote zilizopelekea kutokea maafa hayo na wahusika wa kosa hilo la kusikitisha watafuatiliwa na sheria na matokeo ya uchunguzi huyo litaelezwa taifa la Iran na familia za wahanga wa ajali hiyo.

Kwa upande wake, Dk Mohamad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema leo katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, kosa la kibinadamu lililotokea wakati kama huo wa vitisho vya Marekani ndiyo sababu kuu ya ajali hiyo.

Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Iran leo Jumamosi imetoa taarifa rasmi na huku ikiashiria vitisho vya rais wa Marekani na majenerali wa kijeshi wa nchi hiyo vya kushambulia maeneo kadhaa muhimu ndani ya ardhi ya Iran sambamba na kuongezeka ndege za kijeshi za magaidi wa Marekani zilizokuwa zinaruka wakati huo karibu na Iran, katika mazingira kama hayo, kulitokea kosa la kibinadamu lililopelekea kutunguliwa ndege hiyo baada ya kukaribia sana katika kituo kimoja nyeti cha kijeshi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

..........
340