Main Title

source : ParsToday
Jumapili

12 Januari 2020

08:13:24
1001576

Shakhsia wa kisiasa, kiutamaduni na Waislamu nchini Afrika Kusini wamemkumbuka, kumuenzi na kumuomboleza Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH).

(ABNA24.com) Shughuli ya kumuenzi na kumuomboleza kamanda huyo shupavu wa Kiislamu ilifanyika jana Ijumaa katika mji mkuu wa Afrika Kusini Cape Town.

Baadhi ya shakhsia waliohutubia katika marasimu hayo ya kumuenzi Luteni Jenerali Qassim Soleimani walibainisha historia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kusaidia harakati za wananchi Asia Magharibi pamoja na kukabiliana na siasa za kivamizi za Marekani na utawala haramu wa Israel.

Kadhalika washiriki hao wamethamini na kuenzi mchango wa Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzui ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) na  Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq la Al-Hashdu-Sha'abi  na taathira ya kuuawa kwao shahidi katika kuleta umoja baina ya Waislamu.

Ikumbukwe kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu wa Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq al-Hashd al-Shaabi pamoja na wenzao wengine wanane waliuliwa shahidi usiku wa kuamika Ijumaa ya tarehe tatu Januari 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na utawala wa kigaidi wa Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

..........
340