Main Title

source : ABNA
Jumapili

12 Januari 2020

08:26:18
1001578

Shiriki katika kupinga matukio ya kigaidi ya serikali ya Marekani kwa kuweka saini ya digitali

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kampeni ya kulaani mauaji ya kigaidi ya serikali ya Marekani kwa kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Kamanda Qassim Soleimani na Abumahdi Almuhandisi na waambata wao, imeanza rasmi katika mitandao kwa kuweka saini ya digitali.

Kampeni ya kulaani mauaji ya kigaidi ya serikali ya Marekani yaanzishwa  katika mitandao kwa kuweka saini ya digitali

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Kampeni ya kulaani mauaji ya kigaidi ya serikali ya Marekani kwa kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Kamanda Qassim Soleimani na Abumahdi Almuhandisi na waambata wao, imeanza rasmi katika mitandao kwa kuweka saini ya digitali.

Wanaopenda kushiriki katika kampeni hiyo wanaweza kuingia kwa kubofya hapa ambapo kwa kutia saini ya digitali inamaana kuwa unataka Marekani ichukuliwe hatua kwa mauaji yaliofanya.

Aidha inaelezwa  kwamba Kamanda Haji Qassim Soleimani, akiwa ni kamanda mkuu wa majeshi ya Quds ambayo iko chini ya jeshi la kulinda mapinduzi ya Kiislamu ya Iran pamoja na Abumahdi Almuhandisi ambaye ni msaidizi wa kikundi cha majeshi ya wananchi wa Iraq wakiwa pamoja na waambata wao wanane tarehe tatu Januari mwaka huu waliuwawa kwa mashambulizi ya anga yaliofanywa na majeshi ya Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.

Wizara ya ulinzi na usalama ya Marekani ilitangaza kuwa shambulio hilo limefanywa baada ya amri iliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump, ambapo kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya serikali ya Mapinduzi ya Iran alitangaza maombolezo ya siku tatu kufuatia mauaji hayo ya kikatili.

Miili ya mashujaa Qassim Soleimani na Abumahdi Almuhandisi pamoja na waambata iliagwa na watu wengi katika mji wa Baghdad, Kadhimain, Karbala na Najaf ambapo siku ya Jumapili ya tarehe tano ikawa imewasilishwa nchini Iran, kadhalika  iliagwa na wananchi wa mikoa ya Ahvaz, Tehran, Qom na mji aliozaliwa wa Kerman ambapo katika mamilioni ya wananchi walihudhuria katika kuaga miili hiyo