Main Title

source : ABNA
Jumatatu

13 Januari 2020

19:14:16
1002102

Mmoja kati ya wahariri na wana nadharia wakubwa wa Marekani amesema kumuua kamanda Qasim Soleimani kwa shambulio la anga la ndege za kimarekani ni hatua ya kigaidi iliokuwa kinyume na sheria za kimataifa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Noam Chomsky ambaye ni katika wahariri mashuhuri nchini Marekani amesisitiza kuwa kumua Kamanda Qasim Soleimani kwa uchache ni moja katika ya mambo yanayohisabiwa kuwa ni ugaidi wa kimataifa au zaidi yake.

Aidha mhariri huyo ambaye tahririr zake zinazingatiwa zaidi, akibainisha kuwa hatua iliochukuliwa ni kinyume na sheria za kimataifa huku akisisitiza kuwa: kanuni za kimataifa kuhusu suala hilo bila shaka ziko wazi kanuni ambayo inasema airuhusiwi kutumia ubabe wa kijeshi katika mambo ya kimataifa isipokuwa katika mambo machache ambayo hayajatolewa mfano.

Noam Chomsky aliendelea kuyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Gazeti la “Hindustan Times” na kusisitiza kwamba kwa mtazamo wangu hakuna alama yoyte inayoashiria kuwa majeshi ya Marekani yataondoka magharibi ya Asia kwa muda wa wiki au miezi ijayo.

Mwisho alimazia kwa kusema kuwa uwepo wa marekani katika ukanda wa mashariki ya kati ndani ya miaka ya hivi karibuni bado gujafifia na sioni ishara yeyote inayoashiria kutokea jambo hilo, pamoja hatuwezi kujua nini kitatoakea, huku akisistiza kwamba marekani siku hadi siku amekuwa akipoteza nafasi yake katika ukanda wa mashariki ya kati, ukilinganisha mwaka 2003 mwaka ambao Marekani ndio ilifikia kilele cha kushika nafasi katika ukanda wa mashariki ya kati baada ya kushambulia Iraq mashambulio ambayo ni kinyume na sheria.

mwisho/290