Main Title

source : ParsToday
Jumanne

14 Januari 2020

08:19:28
1002227

Misimamo ya kugongana ya Washington kuhusu sababu za kumuua kigaidi Luteni Soleimani

Tarehe 3 Januari 2020, Marekani ilifanya jinai na ugaidi mkubwa wa kumuua kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu tena akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq.

(ABNA24.com) Si hayo tu, lakini Marekani ilimuua kigaidi Kamanda Soleimani akiwa katika mapokezi ya kiongozi rasmi wa serikali ya Iraq, ambapo katika shambulizi hilo la kigaidi, Marekani ilimuua pia kiongozi huyo wa Iraq na wote waliokuwa wamefuatana nao. Serikali ya kibeberu ya Marekani ilijaribu kuhalalisha jinai yake hiyo kwa kudai kuwa eti Kamanda Soleimani alikwenda nchini Iraq kupanga shambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani.

Akihojiwa na televisheni ya Fox News ya Marekani, rais wa nchi hiyo, Donald Trump alijaribu kuhalalisha jinai yake hiyo kwa kusema: Iran ilikuwa inapanga kufanya shambulio kubwa. Ninapenda kufichua kwamba, kuna uwezekano, Iran ilipanga kushambulia balozi nne za Marekani ukiwemo wa mjini Baghdad. Hata hivyo madai hayo ya uongo yasiyo na kichwa wala miguu hayakupata wanunuzi, bali yamepingwa vikali kote ulimwengu hasa ndani ya Marekani kwenyewe. Siku ya Jumapili ya tarehe 12 Januari, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper alikanusha madai ya Trump ya kwamba Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa amepanga kushambulia balozi za Marekani na kusema kuwa, yeye kama waziri wa ulinzi wa Marekani, hana ushahidi wowote wa kuonesha kuwa, Iran ilikusudia kushambulia balozi nne za Marekani.

Trump ambaye ni maarufu kwa jina la rais mzandiki na msema uongo, na kama lilivyosema gazeti la Washington Post kwamba tangu mwezi Januri 2017 hadi mwezi Agosti 2019, Trump alisema uongo kwa zaidi ya mara 12,000 (12 elfu) na alitoa madai mengi mno yasiyo ya msingi wala mashiko, katika kujaribu kuhalalisha jinai yake yaani kitendo chake cha kutoa amri ya kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Suleimani na wote aliokuwa amefuatana nao, hivi sasa pia ameendeleza mbinu yake ile ile ya kusema uongo. Ukiachilia mbali hatua ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani ya kukanusha madai ya uongo ya Trump, swali linalojitokeza hapa ni kwamba, je, Trump ametoa ushahidi wowote wa kuthibitisha madai yake kwamba Luteni Jenerali Soleimani alikusudia kushambulia balozi za Marekani, au madai yake hayo ni sawa na mamia ya madai yake ya uongo na yasiyo na msingi anayoyatoa kama sehemu ya vita vya kisaikolojia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuichafulia jina Tehran?

Kusema kweli serikali ya Trump kwa karibu mwaka mmoja na nusu ilikuwa inapanga njama za kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na ilikuwa inasubiri fursa tu ya kufanya jinai yake hiyo. Majasusi wa Marekani walipata taarifa ya safari ya Luteni Soleimani nchini Iraq ambayo kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul-Mahdi al-Muntafiki, Kamanda Soleimani alikwenda nchini Iraq kwa ajili ya kukabidhi barua ya majibu ya Iran kwa barua ya Saudi Arabia, ikiwa ni katika juhudi za Baghdad za kupunguza mivutano baina ya Tehran na Riyadh. Nia hiyo ya kikatili ya Trump imetiliwa nguvu pia na matamshi ya Kamanda Ahmad Vahidi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ulinzi wa Taifa cha Iran aliyesema: Rais wa Marekani ametangaza kwamba Soleimani ilibidi auliwe shahidi tangu miaka miwili nyuma na hata kiongozi mwingine wa Marekani naye alisema kuwa, ilibidi mauaji ya Soleimani yafanyike tangu mwaka mmoja na nusu uliopita, hii ina maana kwamba Wamarekani walikuwa wamepanga tangu zamani kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani ya kukanusha madai ya Trump yanaonesha mgongano mkubwa katika matamshi ya viongozi wa Marekani. Kiujumla ni kwamba viongozi wa serikali ya Trump akiwemo waziri wake wa ulinzi, walikuwa wakidai kuwa wako tayari kufanya mazungumzo na Iran bila ya masharti yoyote, lakini wamefedheheka kwa kukataliwa kikamilifu na Iran ambayo inaishurutisha Marekani irejee kwanza kwenye mazungumzo ya JCPOA ndipo hapo tena kufikiriwe uwezekano wa mazungumzo baina ya Tehran na Washington tena katika kalibu ya mazungumzo ya makubaliano hayo ya kimataifa.

Jinai iliyofanywa na Donald Trump ya kumuua kidhulma mgeni rasmi wa nchi nyingine na baadaye kujifakharisha kwa jinai hiyo, haikuwahi kufanywa na hata marais waliomtangulia Trump, kama George W. Bush na Barack Obama. Na ndio maana Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif akasema: Rais wa Marekani ni mjuba na hana heshima na Mike Pompeo, waziri wake wa mambo ya nje, ndio hana heshima zaidi, wamefanya kosa kubwa la kiistratijia lililotokana na ujinga na kiburi. Wamemuua kidhulma shujaa mkubwa wa vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali, na jenerali mpenda amani zaidi katika eneo hili, (Luteni Jenerali Qassem Soleimani).

...........
340