Main Title

source : ParsToday
Jumanne

14 Januari 2020

08:39:34
1002234

Waziri wa Ulinzi wa Iran: Uungaji mkono wa Iran kwa kambi ya muqawama utaendelea kwa kasi kubwa

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba uungaji mkono wa nchi hii kwa kambi ya muqawama utaendelea kwa kasi kubwa, amesema kuwa katika kipindi cha ukarabati wa Syria, Tehran pia itakuwa pamoja na wananchi na serikali ya nchi hiyo ya Kiarabuu.

(ABNA24.com) Brigedia Jenerali Amir Hatami ameyasema hayo mjini Tehran alipokutana na Ali Abdullah Ayyoub, Waziri wa Ulinzi wa Syria na kubainisha kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inautambua uungaji mkono wake kwa serikali ya Damascus kuwa ni katika wadhifa wa kisheria na kusaidia uthabiti wa eneo.

Akibainisha kwamba kambi ya muqawama hii leo imegeuka na kuwa idolojia na mazungumzo katika eneo, amesema, kitendo cha Marekani cha kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC kimeongeza zaidi hatari ya uwepo wa askari wake katika eneo.

Wazrii wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, makabiliano dhidi ya uwepo wa askari wa Marekani katika eneo  ni lazima yabadilike kuwa mwenendo endelevu na kusimama imara, na amefafanua kwamba, uwezo mkubwa wa Luteni Soleimani ulijikita tu katika kuzuia kupenda makubwa na ubeberu wa madoka ya Magharibi pamoja na utawala haramu wa Kizayuni.

Kwa upande wake Ali Abdullah Ayyoub, Waziri wa Ulinzi wa Syria ameelezea kujitolea kukubwa na kwa ikhlasi kwa Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na kusema kuwa, katika nyanza zote za mapigano dhidi ya magaidi, shujaa huyo mwanamapambano daima alijukumika kama ambavyo binafsi alikuwa pamoja na raia madhlumu wa Syria.

Waziri wa Ulinzi wa Syria ameongeza kwa kusema, Luteni Soleimani alikuwa kiigizo chema kwa vijana wote wanamuqawama na hata wananchi wa Syria na kwamba jina lake litabakia milele katika historia.

Aidha amekabidhi Ngao ya Ushujaa ya Jamhuri ya Kiarabu ya Syria kama zawadi ya juu kabisa inayotolewa na jeshi la nchi hiyo kutoka kwa Rais Bashar al-Assad kwa Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo baadaye itakabidhiwa familia ya Jenerali Qassem Soleimani.

..........
340