Main Title

source : ParsToday
Jumanne

14 Januari 2020

09:19:41
1002242

Nyigo mpya za ufafanuazi wa Nasrullah kuhusu sababu na matokeo ya kuuliwa kigaidi kiongozi wa muqawama

Siku ya Jumapili Sayyid Hassan Nsrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon alizungumzia nyigo mpya za sababu na matokeo ya jinai za serikali ya kigaidi ya Marekani katika kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na watu wengine aliokuwa nao.

(ABNA24.com) Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah alitaja moja ya sababu muhimu za uamuzi wa serikali ya Marekani wa kumuua kigaidi Luteni Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, na kusema kuwa ilitokana na 'utendajikazi' na 'shakhsia ya kuleta umoja' ya shahidi huyo kwa ajili ya mrengo wa muqawama katika eneo.

Kwa upande wa utendajikazi, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa na nafasi muhimu ya ukombozi wa eneo la kusini mwa Lebanon lililokuwa linakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Kizayuni mwaka 2000.

Aidha katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006, alikuwa pamoja na wanamapambano wa Lebanon kwenye medani ya vita, huku akiwa na nafasi athirifu pia katika kuushinda utawala huo pandikizi. Mbali na hayo, Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliongoza mapambano makali dhidi ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) na kuilinda serikali halali ya Syria na kadhalika katika kulinda umoja wa ardhi yote ya Iraq, na hii ni kwa kuwa alishiriki pamoja na wanamuqawama kama vile Abu Mahdi al-Muhandis, katika vita dhidi ya genge hilo la ukufurishaji.

Kwa mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah, shakhsia na utendajikazi wa Haji Qassem Soleimani ni mambo yaliyochangia pakubwa katika kuimarishwa uhusiano wa kidugu kati ya makamanda wa kambi ya muqawama kuanzia Iran, Iraq, Lebanon hadi Syria.

Kwa mujibu wa katibu mkuu huyo wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa 'mbeba bendera ya muqawama katika eneo' kama ambavyo anaweza kutajwa kuwa ni 'kielelezo hai cha shakhsia mwanamapambano.' Umoja miongoni mwa makundi ya muqawama, ndio ulioutia hasira kali utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na Marekani.

Katika sehemu nyingine Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria matokeo ya jinai ya serikali ya Marekani katika kumuua kigaidi kiongozi huyo wa muqawama. Moja ya matomeo muhimu kabisa katika jinai hiyo ya kinyama ya kumuua shahidi Haji Qassem Soleimani na wenzake, ni kufichuka sura halisi ya Marekani.

Kuhusiana na suala hilo Sayyid Hassan Nasrullah anasema: "Kinyume na yale yote iliyoyafanya Marekani katika kipindi cha miaka yote iliyopita, kwa kujaribu kujionyesha kwamba ndio mdhamini wa uthabiti na rafiki wa kuaminiwa katika eneo zima la Asia Magharibi, lakini kitendo cha kumuua kigaidi mwanamapambano huyo kimedhihirisha wazi uhalisia wa Washington. Wakati Marekani inapomuua kamanda wetu mkubwa na ndugu yetu kwa jinai ya namna hiyo, inaonyesha kwamba yenyewe ni shetani mkubwa, kiongozi wa uafriti na mpenda kujitanua kibeberu." Ama matokeo mengine ni radiamali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na jinai hiyo.

Sayyid Hassan Nasrullah alisema kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kwamba radiamali hiyo kupitia shambulizi la makombora dhidi ya kambi ya jeshi la Marekani ya Ayn al Asad nchini Iraq, ni 'kofi' ndogo tu kwenye uso wa Marekani.Kofi hilo kwa mtazamo wa Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon lilikuwa na jumbe tatu muhimu.

 Mosi ni kwamba kofi hilo limethibitisha ushujaa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kushambulia kwa makombora kambi za jeshi la Marekani. Pili ni kuonyesha uwezo mkubwa wa kijeshi wa Iran. Na tatu limetoa ujumbe muhimu kwa Wazayuni ili kuwahafamisha uwezo mkubwa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuwafanya wakome kutoa vitisho vyovyote dhidi ya Iran na mrengo wa muqawama.

Ama sehemu ya tatu ya hotuba ya Sayyid Hassan Nasrullah ni 'stratijia ya kimrengo.' Ukweli ni kwamba Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, aliweka wazi stratijia ya mrengo wa muqawama baada ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani. Kama ambavyo kabla ya hapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alivyosema, stratijia ya muqawama ni 'ulipizaji mkali wa kisasi' na kwamba lengo lake ni kuwatimua askari wa Kimarekani kutoka eneo hili.

Sayyid Hassan Nasrullah pia katika hotuba yake ya siku ya Jumapili alisisitiza kwamba: "Jibu la jinai ya Marekani haikomei katika operesheni moja, bali ni mwenendo mrefu ambao hatimaye utapelekea kutimuliwa askari wote wa Marekani katika eneo."

...........
340