Main Title

source : ParsToday
Jumatano

15 Januari 2020

07:14:36
1002533

Januari 3 mwezi huu, Marekani ilichukua hatua ya kijinai na isiyo ya kisheria ya kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashd al-Shaabi ya Iraq pamoja na watu waliokuwa wamefuatana nao.

(ABNA24.com) Kisingizio cha shambulio hilo la anga la kigaidi kilitajwa kuwa Qassim Soleimani alikuwa akipanga njama za kushambulia ubalozi wa Marekani.

Pamoja na hayo, nyaraka mpya pamoja na matamshi ya viongozi wa ngazi za juu wa Marekani yanaonyesha kuwa, Washington ilikuwa imepanga mauaji hayo miezi kadhaa nyuma na ilichokuwa ikisubiri ni wakati mwafaka tu wa kutekeleza jinai hiyo. Kanali ya Televisheni ya NBC ya Marekani Jumatatu ya juzi ilitoa ripoti inayosema kuwa, Donald Trump alitoa amri yenye masharti ya kuuawa Qassim Soleimani Juni mwaka 2019 yaani miezi saba iliyopita. Ripoti hiyo inaeleza kwamba, baada ya ndege ya ujasusi ya Marekani ya Global Hawk kutunguliwa na Iran, Trump alitoa amri inayosema kuwa, kama mashambuulio ya vikosi vya Iran au makundi yanayofuungamana nayo yatapelekea kuuawa wanajeshi au raia wa Marekani, basi vikosi vya Washington vitamuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani.

Hii ni katika hali ambayo, Jumapili iliyopita Trump alidai bila ya kutoa ushahidi wowopte kwamba, sababu ya kuuawa Qassim Soleimani ni kwamba, alikuwa amekaribia kuwa tishio kwa vikosi vya Marekani na kwamba, eti alikuwa akipanga mikakati ya kuzishambulia balozi nne za Iran.

Wakati huo huo, katika matamshi yake mapya katika uwanja huo, Jumatatu ya juzi Trump alisisitiza kwa jeuri kabisa kwamba, kuuawa Qassim Soleimani aliyemtaja kuwa gaidi nambari moja wa dunia kulipaswa kufanyika miaka 20 iliyopita.

Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, hivi Trump ana ushahidi wowote wa kuthibitisha madai yake hayo au ni kama ilivyo kwa mamia ya madai yake ya huko nyuma ambayo msingi wake ni vita vya kisaikolojia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vyenye lengo la kuichafua Iran?

Suala muhimu ni kwamba, katika hali ya hivi sasa serikali ya Trump inafuata utendaji huo huo kuhusiana na Russia na China. Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amesema kuwa, kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani ni sehemu ya mkakati mpana wa kujilinda dhidi ya changamoto zinazosababishwa na maadui wa Washington na hili linajumuuishwa pia kwa China na Russia.

Donald Trump amedai kwamba, Wademokrats wanamtetea Luteni Jenerali Qassim Soleimani kwa ajili ya kufuatilia malengo yao ya kisiasa na kueleza kwamba, jambo hilo ni fedheha kubwa kwa Marekani.

Matamshi hayo ya Trump yanaashiria msimamo wa Adam Schiff, Mwenyekiti wa Kamati ya Upelelezi ya Kongresi ya Marekani ambaye amesema kuwa, Rais wa nchi hiyo Donald Trump ametoa ripoti za uongo ili kuhalalisha mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Akizungumza Jumatatu ya juzi ya tarehe 13 Januari, Mwenyekiti wa Kamati ya Upelelezi ya Kongresi ya Marekani aliashiria mahojiano ya Donald Trump na televisheni ya Fox News na kusema: Trump na maafisa wengine wa serikali yake wanasema uongo ili kuhalalisha mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Adam Schiff alisema kuwa, kile ambacho Trump na watu wa karibu yake wanachokifanya ni kutia chumvi katika kadhia ya mauaji ya Jenerali Soleimani kwa shabaha ya kuhalalisha mauaji yake na suala hili yumkini likatuburuta katika vita na Iran, jambo ambalo ni hatari kubwa.

Viongozi wa ngazi za juu wa serikali ya Trump wamedai mara chungu nzima kwamba, wamechukua hatua ya kumuua Jenerali Qassim Soleimani ikiwa ni "kinga kabla ya tukio" hasa kwa kuzingatia kukaribia tishio tarajiwa kuhusiana na mipango ya kushambuliwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na balozi nyingine za Washington. Hata hivyo imefahamika wazi kwamba, Trump alitoa amri ya kuuliwa Soleimani miezi kadhaa nyuma.

Ukweli wa mambo ni kuwa, Luteni Jenerali Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandis walikuwa vizingiti na vizuzi vya malengo ya Marekani katikka eneo la Asia Magharibi. Kwa mtazamo wa timu ya usalama wa taifa ya Trumpni kuwa,  mauaji hayo ilikuwa fursa ambayo haikupaswa kuipoteza.  Kimsingi ni kuwa, siyo George W. Bush wala Barack Obama Marais waliotangulia wa Marekani ambao walipata uthubutu wa kutenda jinai kama hii wakichelea matokeo yake mabaya. Hata hivyo Donald Trump ambaye amethibitisha kwamba hatabiriki, amechukua hatua hiyo ya kijinai na kupuuza madhara ya hatua hiyo.

Pamoja na hayo, serikali ya Trump baada ya shambulio la hivi karibuni la kulipiza kisasi la Iran dhidi ya kambi ya kijershi ya Marekani ya Ain al-Assad nchini Iraq inapaswa kuupa uzito uwezo wa kijeshi wa Iran na daima iwe na kitete na hofu kwa hatua nyingine za ulipizaji kisasi za Iran na waitifaki wake wa eneo.

............
340