Main Title

source : ParsToday
Jumatano

15 Januari 2020

07:14:36
1002535

IRGC: Watu milioni 25 walishiriki katika shughuli ya mazishi ya Shahidi Qassem Soleimani

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: " Watu milioni 25 walishiriki katika shughuli ya mazishi na kuuaga mwili wa Shahidi Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC, katika miji ya Ahvaz, Mashhad, Tehran, Qom na Kerman nchini Iran."

(ABNA24.com) Akizungumza Jumanne katika kikao cha kumuenzi Luteni Jenerali Shahidi Qassem Soleimani, Brigedia Jenerali Ramadhan Shariff, Msemaji wa IRGC ameongeza kuwa: "Ushiriki huo mkubwa ni ujumbe wa wazi kwa Marekani kuwa watu wa Iran wana umoja katika kukabiliana na Marekani na wanataka IRGC iipe Marekani pigo katika nyuga zote."

Brigedia Jenerali Shariff ameongeza kuwa, mustakabali wa Asia Magharibi ni ule ambao utashuhudia Marekani ikiondoka katika eneo na nchi pamoja na mataifa yote makubwa ya eneo hili kuweza kujitegemea kikamilifu. Hali kadhalika amesema hatua ya mwisho ya uhuru kamili wa mataifa ya eneo la Asia Magharibi itakuwa ni kuangamizwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kukombolewa taifa la Palestina.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine wanane, walishambuliwa tokea angani na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote wakauawa shahidi katika tukio hilo.

Kufuatia ugaidi huo wa Marekani usiku wa kuamkia Jumatano 8 Januari, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC lilizipiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za Marekani nchini Iraq ikiwa ni kujibu jinai ya kigaidi iliyofanywa na askari vamizi wa Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

............
340