Main Title

source : ParsToday
Jumatano

15 Januari 2020

07:37:49
1002536

Waislamu wa Ivory Coast wamefanya kikao cha kumuenzi na kumkumbuka Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mashahidi wenzake waliouawa hivi karibuni na askari magaidi wa Marekani nchini Iraq.

(ABNA24.com) kikao hicho cha kumuomboleza Jenerali Soleimani na mashahidi wenzake kilifanyika usiku wa kuamkia jana Jumatatu katika Msikiti wa Ithnaashari katika eneo la Markouri ulioko katika mji mkuu wa kiuchumi wa nchi hiyo Abidjan.

Washiriki wa kikao hicho wametuma salamu za rambirambi kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, serikali na taifa la Iran kwa ujumla, kwa kuondokewa na shujaa huyo wa muqawama.

Aidha wametoa mkono wa pole kwa makundi na harakati zote za muqawama kote duniani, kwa kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, na mashahidi wenzake.

Waislamu wa Kodivaa walioshiriki mkutano huo katika Msikiti wa Ithnaashari mjini Abidjan wamemtaja Haji Soleimani kama shujaa na mwanamapambano aliyesabilia maisha yake katika harakati na jitihada za kuyatokomeza makundi ya kigaidi hususan Daesh (ISIS) katika eneo la Asia Magharibi.

Kadhalika washiriki wa kikao hicho wakiwemo waandishi wa habari mashuhuri wa Ivory Coast wameilaani Marekani kwa kutekeleza ugaidi huo dhidi ya Soleimani, na kisha kuihadaa dunia kwa kujaribu kuhalalisha jinai hiyo.

Wiki iliyopita, kundi la Maimamu wa Kisunni na Kishia pamoja na wanafunzi na wanachuo nchini Ivory Coast walikusanyika katika ubalozi wa Iran nchini humo, kutoa mkono wa pole kwa taifa la Iran kufuatia mauaji ya kigaidi ya Jenerali Soleimani katika ardhi ya Iraq.

..........
340