Main Title

source : ABNA
Jumamosi

18 Januari 2020

21:18:35
1003452

Mkuu wa mahakama za jinai katika mji wa Nuremberg: mauaji ya Qasim Soleimani ni hatua iliokuwa kinyume na Sheria na maadili.

Serikali ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kuwa walichukua hatua ya kumuua kamanda Qasim Soleimani kwa mujibu wa amri iliotolewa na Rais wa Marekani, mimi nikiwa kama msomi niliohitimu katika masuala ya kisheria katika chuo kikuu cha Harvard, ambapo nimeandika makala nyingi sana kuhusu masuala ya kisheria, hivyo nasema bila ya kusita kuwa mauaji yaliofanyika ni kinyume na maadili na kanuni za kitaifa na kimataifa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Hayo yamesemwa na mkuu wa mahakama ya makosa ya jinai ya katika mji wa Nuremberg amesema mauaji ya kikatili yaliofanyika dhidi ya Kamanda Qasim Soleimani kufuatia amri ya Trump ni hatua iliokuwa kinyume na maadili na sheria.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Asriran imenukuu kauli ya mwanasheria huyo wa Kimarekani aliokuwa ana umri wa miaka mia moja kauli yake imenukuliwa katika gazeti la kimarekani la New York Times ambapo mwanasheria huyo alisema: kwa sasa nimeangia katika mwaka wa mia moja katika maisha yangu na siwezi kulinyamazia suala hili. Mnamo mwaka 1921 nilikuja Marekani kama muamiaji aliokuwa masikini, nahisi kuwa ni wadhifa wangu kulipa wema niliotendewa na serikali ya Marekani.

Katika vita ya pili ya Dunia nilikwenda vitani nikiwa kama mwanajeshi ya Marekani pia najifaharisha kuwa baada ya vita kuisha nikawa hakimu mkuu wa mahakama ya makosa ya jinai ya Nuremberg, ambapo niliwahukumu viongozi wa Nazi ambao walifanya mauaji ya mamilioni ya wanauni na wanawake na watoto wasiokuwa na makosa nk.

Serikali ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kuwa walichukua hatua ya kumuua kamanda Qasim Soleimani kwa mujibu wa amri iliotolewa na Rais wa Marekani, mimi nikiwa kama msomi niliohitimu katika masuala ya kisheria katika chuo kikuu cha Harvard, ambapo nimeandika makala nyingi katika kombi yangu, hivyo nasema bila ya kusita kuwa mauaji yaliofanyika ni kinyume na maadili na kinyume na kanuni za kitaifa na kimataifa

Wananchi wana haki ya kujua ukweli wa suala hili, hivyo basi taasisi za kimataifa, mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, wahusika wa masuala ya kisheria zote zimewekwa mbali katika kadhia hiyo. Lakini katika ulimwengu huu wa sasa vijana ndio wako katika hatari zaidi, isipokuwa pale tutakapoweza kubadili nyoyo za watu ambao huifanya vita kuwa ndio kanuni.

mwisho/290