(ABNA24.com) Timu hizo zimetangaza uamuzi huo leo na kusisitiza katika taarifa yao kwamba: Hazitatii uamuzi huo wa kiuonevu uliochanganyika na matashi ya kipropaganda dhidi ya hali ya usalama ya Iran.
Katika barua kwa Shirikisho la Soka la Iran, Shirikisho la Soka la Asia limetangaza kuwa, kamati ya utendaji ya shirikisho hilo inakusudia kuandaa mechi za timu za Iran na washindani wao katika nchi isiyoelemea upande wowote.
Kisingizio kilichotumiwa na Shirikisho la Soka la Asia kuchukua uamuzi huo wa kiafriti ni kutokuwepo amani na usalama nchini Iran.
..........
340