Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

20 Januari 2020

09:15:20
1003911

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, hali ya sasa ya eneo la magharibi mwa Asia ni ya hatari sana na kwamba Marekani ndiyo sababu kuu ya hali hiyo.

ABNA24.com) Muhammad Javad Zarif amekiambia kituo cha habari cha Timesnow cha India kwamba, misimamo ya kiburi na kijuba ya Marekani ndiyo sababu kuu ya hali hatari ya sasa katika eneo la magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa, Washington inayaangalia mambo yote ya eneo hilo kupitia miwani yake na si miwani na mitazamo ya watu wa magharibi mwa Asia.

Zarif ameashiria uungaji mkono mkubwa wa watu wa nchi za kanda hii ya Asia magharibi kwa Luteni Jenerali Qassem Soleimani  aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) na kusema: Marekani inapaswa kuelewa kuwa baada ya mauaji yake ya kigaidi dhidi ya Jenerali Soleimani sasa watu wa maeneo tofauti ya dunia wanakusanyika kumkumbuka na kumuenzi shujaa huyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kundi la kigaidi la Daesh, Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mike Pompeo pekee ndio waliofurahishwa na mauaji ya kigaidi ya Jenerali Soleimani.
Itakumbukwa kuwa,  usiku wa  kuamkia Ijumaa ya Januari 3 serikali ya Marekani ilifanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al-Muhandes Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (al Hashdu al Shaabi).

............
340