Main Title

source : ParsToday
Jumatatu

20 Januari 2020

09:32:17
1003918

Muhammad Muhyi: Wanajeshi wa muungano wa Marekani wanapasa kufikiria kuondoka Iraq

Msemaji wa Brigedi za Harakati ya Hizbullah ya Iraq ameunga mkono uamuzi wa bunge na serikali ya Iraq wa kuwafukuza nchini humo wanajeshi magaidi wa Marekani na kueleza kuwa wanajeshi wa Marekani na wale wa muungano vamizi wanapasa kufikiria kuondoka Iraq.

(ABNA24.com) Muhammad Muhyi ameongeza kuwa watoto wa Iraq wataendeleza juhudi za kuhitimisha uwepo kinyume cha sheria wa wanajeshi wa Marekani nchini kwao na kwamba Hizbullah ya Iraq itaendeleza kwa nguvu harakati zake katika nyuga za kisiasa, kijamii na nyinginezo baada ya Marekani kuiweka katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Wabunge wa Iraq tarehe 5 mwezi huu wa Januari walipasisha mpango wa kuwafukuza nchini humo wanajeshi wa Marekani kufuatia kuuliwa kigaidi na serikali ya kigaidi ya Marekani Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Harakati ya al Hashd al Sha'abi ya Iraq. Wabunge wa Iraq walipiga nara za 'Mauti kwa Marekani' na 'Mauti kwa Israel' wakati wa kuanza kikao hicho.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis na wenzao wanane waliuawa shahidi alfajiri ya Ijumaa ya tarehe tatu Januari katika shambulio la anga la magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.

Nchi, taasisi na makundi mengi yalilaani kitendo hicho cha kigaidi cha Marekani. Kamanda Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis ni miongoni mwa shakhsia watajika katika vita dhidi ya makundi ya kitakfiri na kigaidi likiwemo kundi la Daesh katika eneo la Asia ya Magharibi. 

..........
340