Main Title

source : ABNA
Jumatano

22 Januari 2020

05:20:09
1004333

Qasim Soleimani

Balozi wa Yemen nchini Iran awasili nyumbani kwa Kamanda Qasim Soleimani+ picha

Balozi wa serikali ya Yemen mjini Tehran amewasili nyumbani kwa jemedali Kamanda Qasim Soleimani na kuonana na familia ya kamanda huyo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Ibrahim Ad`dailami” Balozi wa Yemen nchini Iran akiwa pamoja na “Adnani Ghaflah” msimamizi wa masuala ya kimataifa katika kikundi cha Ansarullah, wamewasili nyumbani kwa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la Quds Jeneral Shahid Qasim Soleimani na kutoa mkono wa Pole alkadhalika kufikisha ujumbe wa viongozi wakuu wa kikundi cha Ansarullah kwa familia hiyo.

Aidha balozi wa Yemen nchini Iran amitoa mkono wa pungezi na rambirambi kwa kifo cha kishujaa cha kamanda Qasim Soleimani kwa familia yake pia kuwasilisha salamu na rambirambi kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha Ansarullah (Abdulmalik Alhuthiy” na Mahdi Almashati “msimamizi wa kamati kuu ya kisiasa nchini Yemen” kwa familia hiyo.

Balozi wa serikali ya Yemen mjini Tehran amesema kuwa kumpoteza kamanda Qasim Soleimani imekuwa ni hasara kubwa kwa uma wa Kiislamu, ambapo wananchi wa Yeman walifanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo na baadhi ya mikoa kwaajili ya kuguswa na msiba huo mkubwa.

Mwisho alimaliza mazungumzo yake kwa kusema kwamba maandamano ya wananchi wa Yemen ni kwaajili ya kuonyesha kuwa wako pamoja katika kukabiliana na mipango ya hujuma za kizayuni na kimarekani na kusisitiza kuwepo umoja na mshikamano katika kukabiliana na suala hilo, huku akitoa upanga wa kiyemen ikiwa ni kama zawadi kwa mtoto wa Qasim Soleimani na familia yake kwa ujumla.

mwisho/290