Main Title

source : ABNA
Jumatano

22 Januari 2020

06:43:55
1004384

Heshima maalumu yatolewa na wachezaji wa mpira wa mikono katika mashindano ya Asia

Timu ya taifa ya mpira wa mikono nchini Iran imetoa heshima maalumu kambla ya kuanza mashindano hayo yanayofanyika nchini Kuwait ilipokuwa ukiimbwa wimbo wa taifa wa Iran huku wakiwa wameshika bendera ya Iran na kutoa heshima hizo kwa mtindo wa kijeshi

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: timu ya taifa ya Iran ikiwa katika mashindano ya mpira wa mikono ya washindi wa Asia yanayofanyika nchini Kuwait imetoa heshima maalumu kwa mtindo wa kijeshi mbele ya watazamaji zaidi ya elfu 10 ambapo mpaka mwisho wa mchezo huo timu ya Iran ilishinda 28 kwa 24 dhidi ya timu ya taifa ya Kuwait.

kutoa heshima hiyo mbele ya bendera ya taifa ya Iran, maana yake ni kujitambulisha kuwa wao ni wanajeshi wa Iran wanaopambana kulitetea taifa hilo, picha za tukio hilo zimeshabikiwa kwa kiasi kikubwa katika mitandao ya kijamii na mwisho wa mchezo huo kingozi wa mpira wa mikono nchini Iran “Ali Riza Pakdel” alisema kuwa ushindi huo umepatikana kwa baraka za roho ya mtakatifu Shujaa Qasim Soleimani.

mwisho/290