Main Title

source : ParsToday
Jumatano

22 Januari 2020

09:38:20
1004438

Vyombo vya habari vya Marekani vimefichua kwamba, madai yaliyotolewa na rais wa nchi hiyo, Donald Trump kwamba Iran ilikuwa na nia ya kushambulia balozi nne za Marekani yamewashangaza na kuwaacha bumbuazi hata washauri wake mwenyewe.

(ABNA24.com) Kikiripoti kuhusu madai ya Donald Trump kwamba Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa akipanga mashambulizi dhidi ya balozi nne za Marekani, madai ambayo yalitumiwa na kiongozi huyo kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya jenerali huyo, kituo cha habari cha The Daily Beast kimeandika kuwa: Matamshi hayo ya Trump yamewastaajabisha na kuwaacha bumbuazi hata wajumbe wa timu ya usalama wa taifa ya White House na washauri wake mwenyewe.

The Daily Beast imeongeza kuwa: Wakati Trump alipotoa madai hayo, maafisa wa ngazi za juu wa timu ya usalama wa taifa ya serikali ya Marekani walitikisa vichwa na hawakujua ni kwa nini rais anafanya propaganda kama hizo.

Ripoti ya The Daily Beast inasema, baada ya madai hayo ya Donald Trump wajumbe wa timu ya usalama wa taifa ya Marekani walikabiliana na mawimbi makali ya maswali ya vyombo vya habari na baadhi yao walisema waziwazi kwamba, Trump amepotosha ripoti zao.

Madai yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani kuhalalisha mauaji ya kigaidi ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya Jenerali Qassem Soleimani yamezusha maswali mengi katika vyombo vya habari kwa kadiri kwamba, hata Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Mark Esper amelazimika kukiri kwamba, hana taarifa yoyote kuhusiana na vitisho vya kushambuliwa balozi nne za Marekani nje ya nchi.    

...........
340