Main Title

source : ABNA
Jumatano

22 Januari 2020

20:00:51
1004625

kamanda Qasim Soleimani

Wanachuo wa chuo kikuu cha Aligarh cha India waandamana kupinga mauaji ya Qasim Suleimani

Wanafunzi wa wa chuo kikuu cha Aligarch nchini India wameandamana kupinga mauaji ya kigaidi dhidi ya kamanda Qasim Soleimani na wenzake yaliofanywa na serikali ya Marekani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Wanachuo wa chuo kikuu cha Aligarch nchini India wameandamana kupinga mauaji ya kigaidi dhidi ya kamanda Qasim Soleimani na wenzake yaliofanywa na serikali ya Marekani.

Wanachuo hao walikuwa wamebeba picha za Kamanda Qasim Soleimani na Abumahdi Almuhandisi pamoja na mabango mbalimbali yanayoashiria kupinga vikali mauaji ya Qasim Soleimani na wenzake huku wakiitakia kuangamia kwa serikali ya Marekani.

Moja kati ya mabango yao iliandikwa “kifo cha kishujaa ni moja kati vitu vinavyomzindua wanadamu” bango lingine liliandikwa “ kadiri utakapotuuwa mataifa yetu ndio yatazidi kuzinduka” nk.

Ripoti zinasema kuwa mnamo tarehe tatu mwezi wa kwanza mwaka huu aliuliwa Kamanda Qasim Soleimani na Abumahdi Almuhandisi na wenzao waliokuwa pamoja nao, kufuatia shambulio la ndege za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, ambapo shirika la kijasusi la Marekani lilitangaza kuwa mauaji hayo yamefanywa kwa mujibu wa amri iliotolewa na Rais wa Marekan Dunald Truamp.

MWISHO/290