Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

23 Januari 2020

07:39:50
1004746

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kitendo cha adui cha kumuua kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani kilikusudia kupunguza ushawishi wa Iran katika eneo hili lakini Tehran itakuwa imara zaidi na itakuwa na ushawishi mkubwa zaidi baada ya mauaji hayo ya kigaidi.

(ABNA24.com) Sayyid Abbas Mousavi alisema hayo jana na kuongeza kuwa, kumuua kigaidi kamanda huyo mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni hasara isiyofidika, lakini kwa baraka za damu ya shahidi huyo, leo hii kumepatikana mwamko na nguvu mpya katika kona mbalimbali za dunia dhidi ya Marekani.

Amesema, matunda ya kwanza kabisa ya damu ya shahidi Soleimani na wenzake, ni mshikamano uliooneshwa na serikali na wananchi wa Iraq wa kutaka wanajeshi magaidi wa Marekani wafukuzwe nchini humo. Bunge la Iraq limepasisha muswada wa kufukuzwa wanajeshi wa Marekani nchini humo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema, chanzo cha matatizo, mapigano, mivutano na mizozo yote ni uingiliaji wa madola ajinabi katika masuala ya ndani ya eneo hili. Amesisitiza kwa kusema: Kuwepo Marekani na mabeberu wenzake katika eneo hilo hakujaleta matunda yoyote zaidi ya chuki, vita na umwagaji damu za watu wasio na hatia.

Tarehe 3 Januari mwaka huu, jeshi la Marekani lilimuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq tena uraiani. Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Shaabi, Abu Mahdi al Muhandis na wenzao wanane pia waliuliwa kigaidi na wanajeshi wa Marekani katika shambulio hilo la kikatili lililokanyaga sheria zote za kimataifa.

...........
340