Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

23 Januari 2020

07:55:00
1004761

Rais wa Iraq: Kutaka majeshi ya kigeni yaondoke kumetokana na kuvunjiwa heshima mamlaka yetu ya kujitawala

Rais Barham Salih wa Iraq amesema: Miito ya kutaka majeshi ya kigeni (Marekani) yaondoke Iraq ni jibu kwa kitendo cha kuvunjia heshima haki ya kujitawala ya nchi hiyo.

(ABNA24.com) Akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Dunia la Kiuchumi linalofanyika mjini Davos, Uswisi, Salih amebainisha umuhimu na nafasi ya nchi yake katika eneo la Asia Magharibi na kuongeza kwamba: Kuheshimiwa mamlaka ya kitaifa ya kujitawala Iraq ni jambo la lazima na lenye umuhimu mkubwa sana kwa ajili ya kuleta amani na utulivu katika eneo hilo muhimu na la kistratejia.

Amesema, mpango uliopitishwa hivi karibuni na bunge la Iraq wa kutaka majeshi ya Marekani yaondoke nchini humo ni takwa la wananchi wote wa Iraq.

Aidha Rais Barham Salih amemuelezea Ayatullah Sistani, marjaa taqlidi wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq kuwa ndiye sababu ya kuvuka dhoruba na kupiga hatua nchi hiyo kuelekea bandari ya amani na akaongeza kwamba, uchaguzi wa mapema ni fursa muafaka ya kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.

Itakumbukwa kuwa kufuatia jinai ya kinyama iliyofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi ya Iraq pamoja na wasaidizi wao wanane katika uwanja wa ndege wa Baghdad, Iraq usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe 3 ya mwezi huu wa Januari, mnamo Jumapili ya tarehe 5, Bunge la Iraq lilipitisha mpango wa kutaka majeshi ya Marekani yaondoke katika ardhi ya nchi hiyo.

Kamanda shahidi Qassem Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo.

..........
340