Main Title

source : ParsToday
Alhamisi

23 Januari 2020

07:55:02
1004762

Iran na Saudia ziko tayari kwa mazungumzo ya kutatua mivutano katika uhusiano wa pande mbili

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia kila moja imetangaza kuwa iko tayari kufanya mazungumzo kwa ajili ya kutatua mivutano iliyopo katika uhusiano wa pande mbili.

(ABNA24.com) Kanali ya televisheni ya Al Mayadeen imemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al-Saud akieleza kwamba, nchi nyingi zimependekeza kuwa wasuluhishi kwa ajili ya mazungumzo kati ya Riyadh na Tehran na akasisitiza kuwa, Saudia iko tayari kufanya mazungumzo na Iran.

Wakati huo huo Mahmoud Vaezi, mkuu wa ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaeleza waandishi wa habari pembeni ya kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri kwamba, Iran inakaribisha wazo la kuboresha uhusiano wake na Saudi Arabia.

Ameashiria kuwa, huko nyuma ulikuwepo uhusiano mzuri kati ya Tehran na Riyadh na akabainisha kwamba, kutatuliwa mivutano iliyopo katika uhusiano wa Iran na Saudia ni kwa manufaa ya eneo hili.

Kwa mujibu wa ripoti ya Al Mayadeen, katika miezi ya karibuni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimetumiana jumbe kadhaa kwa ajili ya kutatua mivutano iliyopo katika uhusiano wa pande mbili.

Kabla ya hapo pia, Waziri Mkuu wa serikali ya mshikizo ya Iraq Adil Abdul-Mahdi alitangaza kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, alikuwa amebeba ujumbe wa Iran kwa ajili ya mazungumzo na Saudia wakati alipouliwa shahidi katika shambulio la kigaidi lililofanywa na Marekani.

Shahidi Qassem Soleimani, aliyekuwa amesafiri kuelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuawa katika shambulio la anga lililofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.

.........
340