Main Title

source : ABNA
Alhamisi

23 Januari 2020

18:21:36
1004878

kamanda Qasim Soleimani

Riwaya za hamasa za kuuaga mwili wa kamanda Qasim Soleimani zakusanywa sehemu moja

Mitazamo na riwaya za hamasa za wananchi katika kuanga mwili wa kamanda Shahid Qasim Soleimani zakusanywa katika mikoa na miji yote na baada ya hapo zitachapishwa na kusambazwa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Taasisi ya Tablighati Islamiy imeamua kukusanya miono yote inayotolewa na wananchi walioshiriki katika kuuaga mwili wa Kamanda Shahid Qasim Soleimani na Abumahdi Almuhandisi na wafuasi wao na kuyafanya maneno hayo yawe yenye kudumu katika historia.

Kinachokusudiwa katika hatua na maamuzi hayo ni kuacha taswira ya mazingira yaliokuwa katika mikoa na miji na maeneo yaliokuwa yameshiriki kumuaga makamanda hao na wenzake kadhalika hamasa ziliokuwa zikitolewa na walioshiriki katika msiba huo, na kulifanya tukio hilo likumbukwe daima dawama kwa watu watakaokuja baadae.

Hivyo wale ambao watahitaji kushiriki katika zoezi hili, wanatakiwa kufanya kama ifuatavyo, riwaya zao wanapaswa kuziandika kuanzia maneno 1000 hata maneno 4000 na kuyaweka katika faili la Word na kuambatanisha na jina na namba yake ya simu na kuituma katika email: [email protected] na katika mitandao ya kijamii ya Eitaa, Soroush na Telegram kwa anuani hii: revayat_rastakhiz@. Muda wakuwasilisha riwaya yako mwisho wake ni tarehe 1 mwezi wa pili.

mwisho/290