Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

25 Januari 2020

08:14:30
1005245

Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa hatua na chokochoko za kijeshi zinazofanywa na Marekani katika eneo la Asia Magharibi, ndio chanzo cha machafuko ndani ya eneo hilo na ameongeza kuwa, uthibitisho wa mwisho wa jambo hilo ni kumuua kigaidi Luteni Qassem Soleimani katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghadad, Iraq.

(ABNA24.com) Majid Takht-Ravanchi aliyasema hayo Jumatano iliyopita katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo aliashiria kadhia ya Asia Magharibi na Palestina na kusema: “Kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni uthibitisho wa ugaidi wa kiserikali na ukiukaji wa wazi wa misingi ya sheria za kimataifa unaotokana na Marekani kujiona polisi wa dunia.

” Ukweli ni kwamba mienendo ya Marekani ya Trump duniani imeibua migogoro tofauti; na katika hilo eneo la Asia Magharibi limeathiriwa pakubwa na harakati za kisiasa na kijeshi za Marekani.

Matumizi ya ugaidi, uwepo wake kijeshi nchini Iraq na Syria, uungaji mkono kijeshi na kisiasa kwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, na hatua zingine za kijeshi za Marekani, ni mambo yaliyochochea migogoro eneo la Asia Magharibi. Aidha uungaji mkono kwa siasa za vita za utawala haramu wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu hadi uungaji mkono wake kisiasa sambamba na kuzichochea tawala tegemezi za Kiarabu, pamoja na hatua zake za kuzuia ustawi zaidi wa kiserikali na kitaifa nchini Iraq na hatimaye dhihirisho la matukio ya kijeshi la kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, yote hayo yameifanya Marekani ionekane kuwa ni nchi inayochochea machafuko tu katika eneo hili.

Marekani ambayo ipo eneo la Asia Magharibi kwa madai ya kupambana na ugaidi kupitia kile inachodai kuwa ni muungano wa kijeshi wa kupambana na kundi la Daesh (ISIS) nchini Syria, inapora mafuta tu ya nchi hiyo ya Kiarabu kama ambavyo pia imezuia ustawi nchini Iraq na hatimaye ikatekeleza mauaji ya kigaidi dhidi ya kamanda halisi aliyeongoza mapambano ya kutokomeza ugaidi na siasa haribifu za Marekani katika eneo.

Matokeo ya siasa hizo haribifu za Marekani hayakuwa na faida nyingine ghairi ya kuendeleza ghasia na machafuko katika eneo, na matokeo yake ikawa ni kuharibu njia athirifu ya kudhamini usalama na amani ya eneo na hivyo kutakiwa kuondoa askari wake.Hii leo kitendo cha kumuua kigaidi Luteni Jenerali Soleimani, kimeandaa zaidi mazingira ya kutimuliwa askari wa Kimarekani katika eneo hili kuliko wakati mwingine wowote ule, na hii ni kwa kuwa fikra za walio wengi katika nchi za eneo la Asia Magharibi ikiwemo Iraq, zimebainikiwa na uhalisia wa ugaidi wa Marekani hasa baada ya kutekeleza jinai dhidi ya kamanda huyo wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC.

Marasimu ya mamilioni ya watu katika kuusindikiza na kuuaga mwili wa Luteni Jenerali Qassem Soleimani nchini Iraq na Iran na kadhalika shughuli za kumuenzi shahidi huyo pamoja na mashahidi wengine aliokuwa pamoja nao zilizofanyika katika nchi zote za eneo la Asia Magharibi, yameandaa uwanja wa kutimuliwa askari hao wa Kimarekani sambamba na kuzidisha chuki za raia wa eneo hili dhidi ya Marekani. Ni nadra sana kuipata nchi ya eneo la Asia Magharibi na hata duniani ambayo inaweza kukubali madai ya Marekani kuwa eti Washington inaendesha mapambano dhidi ya ugaidi, hasa baada ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Soleimani aliyekuwa akiongoza mapambano halisi dhidi ya janga hilo la ugaidi. Katika mazingira hayo, hatma ya matokeo ya ulipizaji kisasi kikali kufuatia kuuawa shahidi shakhsia huyo, imetilia mkazo suala la kutimuliwa askari wa Kimarekani katika eneo la Asia Magharibi na hii ndio njia pekee ya kurejesha usalama na amani katika eneo.

...........
340