Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

25 Januari 2020

08:14:30
1005246

Iran: Marekani imedhihirisha sura yake ya kigaidi kwa kutishia kumuua Brigedia Qaani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali matamshi ya kijuba yaliyotolewa na "kundi la kuichukulia hatua Iran" la wizara ya mambo ya nje ya Marekani ya kutishia kumuua kigaidi Brigedia Jenerali Ismael Qaani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.

(ABNA24.com) Hatua hiyo ya Sayyid Abbas Mousavi imekuja baada ya mwakilishi maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran kutoa matamshi ya kijuba akitishia kuwa Marekani itamuua kigaidi pia Brigedia Jenerali Ismael Qaani, aliyechukua nafasi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH aliyeuliwa kigaidi na Marekani wakati akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq karibu na uwanja wa ndege wa baghdad tarehe 3 mwezi huu Januari 2020.

Katika vitisho vyake vipya, Brian Hook mkuu wa kitengo cha kuchukua hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani aliliambia gazeti la al Sharq al Awsat jana Alkhanisi mjini Davos Uswisi kwamba kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, Brigedia Jenerali Ismael Qaani naye atafikwa na hatima ile ile iliyomfika Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, matamshi ya afisa huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ni kutangaza rasmi na hadharani kwamba Washington inaendesha ugaidi wa kiserikali ulimwenguni.

Amesema, ukitoa utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani ni dola dhalimu la pili linalotangaza rasmi kutumia suhula za serikali na majeshi yake kufanya ugaidi.

...........
340