Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

25 Januari 2020

08:14:31
1005247

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, athari za kibao kikali cha uso ambacho vikosi vya ulinzi vya Iran vimeipiga Marekani, zitabakia milele katika historia.

(ABNA24.com) Jenerali Amir Hatami akisema hayo jana Alkhamisi katika kongamano la kwanza la viwango vya majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapa Tehran na kuongeza kuwa, kibao kikali kilichotolewa na vikosi vya ulinzi vya Iran kupitia kushambulia kwa makombora kambi ya Wamarekani ya Ain al Assad huko Iraq kilitimiza viwango vya juu kabisa vya ubora katika upande wa wakati, namna na ustadi wa hali ya juu wa kupiga shabaha makombora ya Iran.

Alisema, wananchi wa Iran ndio waliotaka taifa lao litoe majibu makali kwa jinai za Marekani na kuongeza kuwa, leo hii Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imejiimarisha vizuri katika nyuga zote za kiulinzi na ina azma ya kweli ya kutoa majibu makali kwa mvamizi na mchokozi yoyote tena kwa kwango chochote ya silaha na kwa kiwango cha juu cha kujihami.

Tarehe 8 Januari 2020 Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH lilitoa majibu makali kwa kushambulia kwa makumi ya makombora kambi za kijeshi za Marekani katika mikoa cha al Anbar na Arbil nchini Iraq baada ya wanajeshi magaidi wa Marekani kumuua kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha jeshi la SEPAH wakati akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq tena uraiani.

...........
340