Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

25 Januari 2020

08:32:30
1005253

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amelaani vitisho vilivyotolewa na Marekani vya kumuua kigaidi kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah).

(ABNA24.com) Maria Zakharova amewaambia waandishi habari kwamba, vitisho vilivyotolewa na Marekani kwamba itamuua kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Ismail Qaani haviwezi kukubalika.

Zakharova amesema: Kwa mtazamo wa Moscow, matamshi kama haya yanakiuka sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala ya nchi yoyote huru, na kwamba Marekani haina haki ya kutoa matamshi kama haya.

Katika mahojiano aliyoyafanya Alhamisi na gazeti la Asharq al-Awsat pembizoni mwa mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani huko Davos nchini Uswisi, mkuu wa kitengo cha hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Brian Hook alitoa tishio dhidi ya kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Ismail Qaani.

Afisa huyo wa Marekani alisema kuwa iwapo, Brigedia Jenerali  Qaani atafuata njia ya Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani basi atakuwa na hatima sawa na iliyomkumba kamanda huyo wa zamani wa Kikosi cha Quds cha IRGC.

Luteni Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes waliuawa shahidi mapema leo Ijumaa 3 Januari katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. Jenerali Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ndiye aliyetoa amri ya kuuliwa shahidi Jenerali Qassem Soleimani.

..........
340