Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

25 Januari 2020

08:37:13
1005255

Marekani na ugaidi wa kiserikali; tishio la kumuua kigaidi kamanda mpya wa kikosi cha Quds cha IRGC

Baada ya jinai ya Marekani ya kumuua kinyume cha sheria na kiuwoga Luteni Jenerali Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine wanane mnamo Januari 3 2020 katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Baghdad, sasa utawala wa Trump umetoa tishio jipya la ugaidi.

(ABNA24.com) Brian Hook mkuu wa kitengo cha hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ametoa tishio dhidi ya kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Ismail Qaani. Katika mahojiano siku ya Alhamisi, Hook amekariri madai yasiyo na msingi dhidi ya Shahidi Qassem Soleimani na kutishia kuwa iwapo  Brigedia Jenerali  Qaani  atafuata njia ya Shahidi Luteni Qassim Soleimani basi atakuwa na hatima sawa na iliyomkumba kamanda huyo wa zamani wa Kikosi cha Quds cha IRGC.

Hook katika kuendeleza vitisho vyake vya kutaka kumuua kigaidi Brigedia Jenerali Qaani amedai kuwa, Trump ameamua kuwa atatoa jibu kali kwa hujuma yoyote dhidi ya Wamarekani.

Mkuu huyo wa kitengo cha hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameendelea kutoa matamshi ya kijuba na kudai kuwa: "Hili si tishio jipya!. Trump anasisitiza kuwa daima yuko tayari kutoa jibu la haraka na kali katika kulinda maslahi ya Marekani."

Kisingizo ambacho Trump alikitumia katika kuamuru mauaji ya kigaidi dhidi ya Luteni Jenerali Soleimani ni kile alichokitaja kuwa ni 'hatari tarajiwa ya kuwahujumu askari wa Marekani" na "Mpango wake wa kushambulia balozi nne za Marekani".  Trump alitoa madai hayo bila kutoa ushahidi wowote na sawa na madai yake mengine, alikuwa analenga kuendeleza vita vya kisaikolojia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  Hii ni katika hali ambayo hata wakuu wa usalama katika Ikulu ya White House na idara zingine za Marekani walibainisha wazi kuwa hawakuwa na taarifa zozote kuhusu madai hayo ya Trump. Wakuu wa usalama wa Washington wamedokeza kuwa, katika kikao na Trump walimfahamisha kuwa balozi za Marekani hazikuwa zinakabiliwa na tishio lolote kutoka kwa Iran.

Kwa maelezo hayo, ni wazi kuwa, kitendo cha Trump cha kumuua Luteni Jenerali Soleimani kimetekelezwa katika fremu ya ugaidi wa kiserikali wa Marekani lengo lilikuwa ni kumuondoa jenerali huyo shujaa Muirani ambaye alikuwa ni kizingiti kikubwa katika kufikiwa njama chafu za Marekani katika eneo la Asia Magharibi. Ushahidi umebaini kuwa, miezi kadhaa iliyopita Marekani ilikuwa imeshachukua uamuzi wa kumuua Haj Qassem Soleimani na kile kilichokuwa kikisuburiwa ni fursa ya kutekeleza jinai hiyo.

Kwa mtazamo wa washauri wa kijeshi na kiusalama wa Marekani,  kuwepo mjini Baghdad kwa wakati mmoja Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis, ambao walikuwa makamanda wawili waandamizi wa Iran na Iraq na waliokuwa na nafasi muhimu na ya kimsingi katika vita dhidi ya magaidi wa ISIS (Daesh), na ambao pia walikuwa ni kizingiti cha utekelezwaji wa njama za Marekani Asia Magharibi, ilikuwa fursa nzuri kwao ambayo haingepaswa kupotezwa. Kwa msingi huo wakuu wa Marekani walitoa amri ya kuuawa makamanda hao wawili, kitendo ambacho ni jinai kubwa ya kivita na ya kiuwoga.

Kwa maelezo hayo, Marekani ilichukua hatua isiyo na kifani ya kumuua kamanda wa ngazi za juu wa kijeshi wa Iran pasina kuwepo mapigano ya kijeshi au kuwepo vita baina ya nchi hizi mbili.

Hatua hiyo ya utawala wa Trump ni mfano wa wazi wa ugaidi wa kiserikali. Nukta nyingine muhimu hapa ni hii kuwa, utawala wa Trump unatekeleza sera sawa na hiyo kuhusu Russia na China.

Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa kitendo cha kumuua Jenerali Soleimani ni sehemu ya stratejia pana ya Marekani ya kukabiliana na changamoto ambazo zinaibuliwa na maadui wa Marekani na hilo linahusu pia China na Russia.

Ni wazi kuwa, Marekani ambayo inajitazama kama mbabe wa dunia, inapuuza sheria na kanuni zote za kimataifa na inaona ni haki yake kutumia nguvu na mabavu dhidi ya nchi zingine na hata kutumia ugaidi wa kiserikali kufikia malengo yake ya kieneo na kimataifa.

..........
340