Main Title

source : ParsToday
Jumamosi

25 Januari 2020

08:39:31
1005258

Hashdu Shaabi: Marekani iondoke Iraq kwa khiari badala ya kusubiri kutimuliwa

Harakati ya kujitolea wananchi ya Hashdu Shaabi ya Iraq imemtaka Rais Donald Trump kuwaondoa wanajeshi wa Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu kwa khiari badala ya kusubiri watimuliwe kwa nguvu.

(ABNA24.com) Qais al-Khazali, msemaji wa harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ambayo ni sehemu ya Hashdu Shaabi amesema hayo katika taarifa na kuongeza kuwa, "hii leo (jana Ijumaa) Wairaqi wote wanawake kwa wanaume wamemiminika mabarabarani kutuma ujumbe mmoja ulio wazi kwa dunia; kwamba hakuna nafasi ya vikosi ajinabi katika ardhi ya Iraq."

Amewashukuru wananchi wa Iraq kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya jana ambayo yalivutia pia wanazuoni wa kidini, shakhsia wa kisiasa, wasomi na hata waandishi wa habari.

Msemaji huyo wa harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ambayo ni sehemu ya Hashdu Shaabi ameongeza kuwa, "kwa mpumbavu Trump, maandamano ya watu milioni moja yanakupa ujumbe ulio wazi, kwamba usipoondoka kwa khiari basi utalazimika kuondoka kwa teke la uso."

Akizungumzia maadamano hayo ya jana ya mamilioni ya watu nchini Iraq, Rais wa nchi hiyo Barham Salih amesema katika ujumbe kwenye Twitter kuwa: Wairaqi wanataka taifa ambalo uhuru wake wa kujitawala haukiukwi, na ambalo masuala yake ya ndani hayaingiliwi na madikteta. Wairaqi wanataka taifa ambalo litawadhaminia wananchi wake usalama, haki, amani na uthabiti katika kuamiliana na majirani."

Naye Mohammad Karim, mwanachama wa muungano wa Fatah katika Bunge la Iraq amesema machaguo yote ya kuviondoa vikosi vya Marekani nchini yapo mezani, iwe diplomasia au mabavu. 

............
340