Main Title

source : ParsToday
Jumapili

26 Januari 2020

09:33:44
1005552

Kiongozi Muadhamu atuma ujumbe kwa Kikao cha 54 cha Umoja wa Jumuia za Kiislamu za Wanachuo wa Ulaya

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwa Kikao cha 54 cha Umoja wa Jumuia za Kiislamu za Wanachuo wa Ulaya akiwasisitizia kwamba, kikao chao mwaka huu kinafanyika baada ya kutokea matukio muhimu na kila moja ya matukio hayo linaonesha ukubwa na itibari ya Iran ya Kiislamu na taifa la kimapinduzi.

(ABNA24.com) Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema katika ujumbe huo ulisomwa jana kwenye kikao hicho mjini Vienna Austria kwamba, kuuawa shahidi watu muhimu, nguvu za kijeshi zilizooneshwa na Jamhuri ya Kiislamu, kujitokeza kwa wingi usio na kifani wananchi katika medani, mioyo imara na isiyotetereka ya vijana wa Iran sambamba na maelfu ya harakati katika nyuga za sayansi na teknolojia na imani ya kidini na kimaanawi katika sehemu kubwa ya vijana kote nchini Iran.

Yote hayo yanaonesha kupata nguvu itikadi ya tauhidi na imani ya Mungu mmoja dunia, itikadi ambayo inaweza kuwa na taathira kubwa mno katika historia ya baadaye.

Aidha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika ujumbe huo kwamba, Awamu ya Pili ya Mapinduzi ya Kiislamu inabidi iifikishe itikadi hiyo katika ukamilifu wake.

Amefafanua kwa kusema: Matumaini makubwa katika kipindi hiki muhimu mno yako kwa vijana wasomi na walioiva kiimani na nyinyi vijana mnaweza kuwa miongoni mwa wateule hao watakaojenga historia.

Kikao cha 54 cha Umoja wa Jumuia za Kiislamu za Wanachuo wa Ulaya kilianza jana Jumamosi huko Vienna, mji mkuu wa Austria.

..........
340