Main Title

source : ParsToday
Jumapili

26 Januari 2020

09:33:45
1005553

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua ya madola ya Ulaya ya kuitii kibubusa Marekani ni maafa na kueleza kwamba, madola ya ulaya hayana ubavu wa kumpinga Rais Donald Trump wa Marekani.

(ABNA24.com) Dakta Muhammad Javad Zarif amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na jarida la kila wiki la Der Spiegel la Ujerumani ambapo sambamba na kuashiria, uwezekano wa nchi tatu za Ulaya za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wa kutumia mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA amebainisha kwamba, madola hayo hayana hoja za kisheria za kutumia mchakato kama huu.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wazi kuwa, Russia na China zina mtazamo mmoja na Tehran na kwamba, madola ya Ulaya yanapaswa kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya vita vikubwa.

Akijibu swali kuhusiana na tishio la Iran la kujitoa katika Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT), waziri Zarif amesema kuwa, kwanza, kujitoa Iran katika mkataba huo hakuna maana ya kutaka kuunda bomu la nyuklia na pili ni kuwa, Iran haina mpango kabisa wa kufanya hivyo kwani hatua hiyo inakinzani za misingi ya kimaadili na kiitikadi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Dakta Zarif ameashiria pia kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani na kusema kuwa, Marekani, Ulaya na jamii ya kimataifa ni wadaiwa wa Qassim Soleimani katika kuangamizwa kundi la kigaidi la Daesh.

..........
340